Vipigo vyampa hofu Lampard

Muktasari:

  • Matokeo hayo ya vipigo ambayo Chelsea inakumbana nayo, yanaendelea kumweka pabaya Lampard ambaye ameifanya timu hiyo kuwa na mwenendo mbaya zaidi chini ya utawala wa Roman Abramovich.

LONDON, ENGLAND. KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard ameanza kuingiwa na hofu juu ya kiwango cha timu yake  kufuatia vipigo ambavyo wamekumbana navyo kwenye michezo mitano  ya Ligi Kuu England kati ya minane iliyopita.

Mabao kutoka kwa Wilfred Ndidi  na  James Maddison yalitosha hapo jana, Jumanne kwa wenyeji wa mchezo huo, Leicester City kuibuka na ushindi wa  mabao 2-0 dhidi ya Chelsea na kukwea hadi kileleni mwa msimamo wa Ligi.

Kutoka kuwa miongoni mwa timu ambazo zilikuwa zikipewa nafasi kubwa ya kuipa changamoto Liverpool kwenye mbio za ubingwa kwa sasa kikosi cha Lampard kipo nafasi ya nane kwenye msimao wa Ligi hiyo wakiwa na pointi 29.

"Hatupo nafasi ambayo tunataka kuwa.Ninashaka kwa sababu ya kiwango tulichonacho kwa sasa, tulishinda dhidi ya Fulham lakini mambo hayakuwa sawa, tunapaswa kuwa bora, kwa asilimi kubwa timu inaundwa na wachezaji vijana hawajisikii vizuri, kila wakati wamekuwa wakipata somo," amesema kocha huyo.

MATOKEO YA CHELSEA MICHEZO 8 ILIYOPITA

Desemba 12, Everton 1-0 Chelsea    
Desemba 15,  Wolves 2-1 Chelsea    
Desemba 21,  Chelsea 3-0 West Ham    
Desemba 26,  Arsenal 3-1 Chelsea    
Desemba 28,  Chelsea 1-1 Aston Villa    
Januari 3,  Chelsea 1-3 Man City    
Januari 16,  Fulham 0-1 Chelsea
Januari 19,  Leicester 2-0 Chelsea