Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vinicius Jr atoa sharti moja Madrid, Waarabu, PSG wajiweka sawa

Muktasari:

  • Mbappe ambaye huu ni msimu wake wa pili akiwa na Madrid analipwa takribani Euro 600,000 kwa wiki wakati Vinicius akilipwa Euro 400,000 kwa wiki.

WINGA wa Real Madrid, Vinicius Jr, 25, amewaambia viongozi wa timu hiyo anataka kulipwa mshahara sawa na ule ambao mshambuliaji mwenzake wa timu hiyo, Kylian Mbappe analipwa na kama takwa hilo halitatimizwa atalazimisha kuondoka mwisho wa msimu huu.

Mbappe ambaye huu ni msimu wake wa pili akiwa na Madrid analipwa takribani Euro 600,000 kwa wiki wakati Vinicius akilipwa Euro 400,000 kwa wiki.

Vinicius amekuwa akihusishwa sana kuondoka hivi karibuni kutokana na hali yake katika kikosi hicho tangu kuwasili kwa kocha mpya Xabi Alonso ambaye mara kadhaa amekuwa akimweka benchi pamoja na kumfanyia mabadiliko kabla ya mechi kumalizika.

Hivi karibuni pia alisikika akitamka hadharani ni bora aondoke kauli ambayo aliitoa baada ya kufanyiwa mabadiliko katika mechi ya El Classico dhidi ya Barcelona.

Waarabu wa Saudi Arabia pamoja na PSG ni miongoni mwa timu zinazoitamani.


Dominik Szoboszla

MANCHESTER City na Real Madrid zote zimevutiwa na kiungo wa Liverpool na timu ya taifa ya Hungary, Dominik Szoboszlai, 25, wanayepanga kumsajili katika dirisha lijalo la majiea ya kiangazi. Szoboszlai ni miongoni mwa wachezaji tegemeo katika kikosi cha Liverpool na vigogo hawa wamevutiwa sana na kiwango chake alichoonyesha tangu ajiunge na Liverpool. Hata hivyo haionekani kama Liverpool itakuwa tayari kumuuza staa huyu kutokana na umuhimu wake.


Kobbie Mainoo

MANCHESTER United ipo tayari kumtoa kiungo wao wa kimataifa wa England,  Kobbie Mainoo, 20, katika dirisha lijalo la majira ya baridi kwa mkopo pekee na sio kumuuza mazima. Mabosi wa mashetani wekundu wanaamini Mainoo ni dhahabu na anaweza akaisaidia timu katika siku za usoni ingawa kocha Ruben Amorim ameonyesha kutokuwa na mpango wa kumtumia akidai anakosa baadhi ya vitu na kuna uwezekano akaondoka huku Napoli ikionekana kummezea mate.


Nicolas Paz

CHELSEA imefanya mawasiliano na Como ya Italia kuulizia uwezekano wa kumsajili kiungo wao na timu ya taifa ya Argentina, Nicolas Paz mwenye umri wa miaka 21, katika dirisha lijalo la majira ya baridi. Paz ambaye pia anawindwa na Real Madrid ambayo ndio inapewa nafasi kubwa ya kumpata anadaiwa kuuzwa kwa takribani Pauni 58 milioni. Kabla ya kutua Como staa huyu alikuwa akiitumikia timuza vijana za Madrid.

Alessandro Baston

LIVERPOOL ipo tayari kulipa Pauni 88 milioni kwenda Inter Milan kumnunua beki kisiki wa klabu hiyo, Alessandro Bastoni. Baston ni miongoni mwa mabeki bora katika Seriea A kwa sasa na kiwango chake kinaonekena kuvutia timu nyingi. Kwa mujibu wa ripoti kutoka Italia, Baston mwenyewe hataki kuondoka kwa sasa na ameshaanza hadi mazungumzo ya kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia Juventus.


Andy Robertson

BEKI wa kushoto wa Liverpool, Andy Robertson, 31, anataka Anfield mwisho wa msimu huu baada ya mkataba wake kumalizika. Robertson anataka kuondoka kwa sababu hapati nafasi ya kutosha kikosi cha kwanza tangu kocha Arne Slot apewe mikoba. Licha ya mkataba wake kuwa umebakisha miezi kadhaa kabla ya kumalizika hadi sasa hakuna mazungumzo yoyote aliyofanya na Liverpool.


Niclas Fullkrug

WOLFSBURG inaangalia uwezekano wa kumsajili straika wa West Ham, Niclas Fullkrug katika dirisha lijalo la majira ya baridi. Staa huyu wa kimataifa wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 22, amekuwa akipitia wakati mgumu katika kikosi cha West Ham na anataka kuondoka hata kwa mkopo ili kujaribu bahati sehemu nyingine.

West Ham ipo tayari kumwachia staa huyu aidha kwa mkopo au kumuuza.


Nicolas Jackson

BAYERN Munich haina mpango wa kukubali ombi la kumrudisha straika wa Chelsea, Nicolas Jackson dirisha lijalo la majira ya baridi na badala yake imepanga kumsainisha mkataba wa moja kwa moja ifikapo mwisho wa msimu huu. Jackson, 24, alijiunga na Chelsea dirisha lililopita na tangu wakati huo amekuwa akionyesha kiwango bora sana.