Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vini Jr kajiweka sokoni, klabu za England zatajwa

VINI Pict

Muktasari:

  • Winga huyo kutoka Amerika Kusini, Vinicius, 25, alitibuana na kocha mpya wa Los Blancos, Xabi Alonso baada ya kumfanyia mabadiliko kwenye mechi ya El Clasico Jumapili iliyopita.

MADRID, HISPANIA: SUPASTAA wa Kibrazili, Vinicius Junior ameziamsha klabu za Ligi Kuu England kwamba yupo tayari kuachana na miamba ya soka ya Hispania, Real Madrid.

Winga huyo kutoka Amerika Kusini, Vinicius, 25, alitibuana na kocha mpya wa Los Blancos, Xabi Alonso baada ya kumfanyia mabadiliko kwenye mechi ya El Clasico Jumapili iliyopita.

Vinicius anamshutumu kocha wake, ambaye ni kiungo wa zamani wa Liverpool na Real Madrid hamtendei vizuri na hampi heshima inayostahili.

Uhusiano wao ulitibuka zaidi wakati Mbrazili huyo alipotolewa uwanjani Bernabeu wakati zikiwa zimebaki dakika 20 mechi ya El Clasico kumalizika na Real Madrid ilifanikiwa kuitandika Barcelona mabao 2-1.

Vini Jr alionekana alishikwa na mshangao wakati anafanyiwa mabadiliko, alirusha mikono kuuliza maswali kwa umma juu ya uamuzi huo wa kocha Alonso kama atakuwa amefanya makosa. Na wakati anatoka uwanjani, kamera ya Spanish TV zilimnasa, akisema: “Mimi? Mimi? Kocha, kocha! Mimi?”

VIN 01

Vinicius kisha aliingia moja kwa moja kwenye korido za uwanjani na alisikika akipiga kelele: “Siku zote ni mimi tu, naondoka hii timu. Naondoka, ni bora niondoke.”

Baadaye alirudi na kukaa kwenye benchi katika dakika za mwisho za mchezo huo.

Na sasa chanzo cha karibu kwa mchezaji huyo kilibainisha jambo hilo limeweka ufa mkubwa baina yake na kocha Alonso na sasa kinachoonekana staa huyo akatimka.

Hilo linaweza kuibua vita kubwa kwenye klabu tajiri za Ligi Kuu England, zikipambana kupata nafasi ya kunyakua mchezaji huyo mwenye kipaji kikubwa cha soka duniani.

Vinicius amefunga mabao 111 katika mechi 316 alizochezea Real Madrid, huku akifunga mabao manane katika mechi 43 alizotumikia timu ya taifa ya Brazil.

Alifunga bao la ushindi kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Liverpool mwaka 2022 na alitikisa nyavu pia wakati Real Madrid iliponyakua taji hilo la ubingwa wa Ulaya mwaka 2024 ilipoichapa Borussia Dortmund uwanjani Wembley.

Real Madrid inamlipa Vini Jr mshahara wa Pauni 350,000 kwa wiki na sasa inamthaminisha staa huyo kuwa na thamani ya Pauni 130 milioni, huku mkataba wake ukifika ukingoni 2027.

VIN 02

Lakini, kutokana na mwenyewe kujiweka sokoni na malumbano yake na Alonso hilo linaweza kuzisukuma timu nyingine kuanza kupeleka ofa wakati wa dirisha la Januari litakapofunguliwa.

Klabu zote za Top Six kwenye Ligi Kuu England zinaweza kuvutiwa na huduma ya Vini Jr. Chelsea na Manchester City ziliwahi kuonyesha dhamira ya kunasa huduma ya Mbrazili huyo huko nyuma, wakati Liverpool kwa muda mrefu imekuwa ikihitaji huduma ya winga wa kushoto.

Man United inaweza kuutazama usajili wa Vinicius kama ni kutuma ujumbe tu kwenye dunia ya soka bado wapo hasa baada ya kumaliza nafasi ya 15 kwenye ligi msimu uliopita.

Arsenal ilionyesha dhamira ya kumsajili mchezaji mwenzake Vini Jr, Mbrazili Rodrygo, wakati ilipoonekana kama angeondoka Madrid dirisha lililopita la majira ya kiangazi kabla ya kuchukua uamuzi wa kumsajili Noni Madueke kutoka Chelsea kwa Pauni 50 milioni.

Wamiliki wa Tottenham Hotspur, familia ya Lewis, imeweka mkwanja wa Pauni 100 milioni kwa ajili ya kuwekeza katika mipango ya muda mrefu ya kimichezo katika klabu hiyo.


MASTAA WALIOFUNIKA KIKOSINI MADRID KWENYE LA LIGA

-Mabao mengi: Mbappe, 11

-Asisti nyingi: Guller, 4

-Pasi nyingi: Carreras, 681

-Krosi nyingi: Guler, 31

-Kupiga tackolin: Valverde, 17

-Faulo nyingi: Mustantuono, 12