Vigogo wa Ulaya watembeza dozi

Beki wa Man u Evra akinyang'anya mpira kwa mshambuliaji
BUCHAREST, Romania MSHAMBULIAJI Wayne Rooney alifunga mabao mawili kwa penalti na kuwaongoza wachezaji 10 wa Manchester United kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Otelul Galati ya Romania katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Rooney alifunga bao la kwanza dakika ya 64, lakini dakika mbili baadaye nahodha wao Nemanja Vidic alitolewa nje kwa kadi nyekundu. Rooney alifunga penalti ya pili katika dakika za majeruhi na kuipa United ushindi wa kwanza katika Kundi C. Real Madrid ilisambaratisha Lyon 4-0 na kuendeleza rekodi yao nzuri msimu huu, mabao hayo ya mabingwa mara tisa yalifungwa na Karim Benzema, Sami Khedira, Mesut Oezil na Sergio Ramos. Mshambuliaji Sergio Aguero aliyeingia kutokea benchi aliifuingia Manchester City bao la ushindi walipoilaza Villarreal 2-1, huo ukiwa ni ushindi kwa kwanza kwa vinara hao wa Ligi Kuu ya England katika Kundi A. Bayern Munich ilipoteza pointi kwa mara ya kwanza katika kundi hilo baada ya kulazimishwa sare 1-1 na Napoli. Inter Milan ilichapa Lille 1-0 na kupanda kileleni mwa Kundi B. Giampaolo Pazzini alifunga bao hilo pekee dakika ya 22 kwa Inter. Katika michezo mingine, Dinamo Zagreb na Basel zote zilipokea vipigo vya mabao 2-0 wakiwa nyumbani kutoka kwa Ajax na Benfica, nayo CSKA Moscow ilichapa Trabzonspor 3-0. Nchini Romania, Otelul pia ilimaliza mchezo huo wakiwa wachezaji 10 baada ya Milan Perendija kutolewa nje kwa kadi nyekundu. “Nafikiri mechi hizi za ugenini ni lazima ufanye kazi kwa sababu si rahisi,” alisema kocha United, Alex Ferguson. “Katika kipindi cha pili tulibadilika na kucheza kwa kiwango kizuri. Nani alicheza vizuri zaidi kipindi cha pili. Nimelizika na matokeo. Ulikuwa ni usiku mgumu na uliohitaji umakini.” Ushindi huo wa kwanza kwa United umewafanya wapande hadi nafasi ya pili wakiwa nyuma kwa pointi mbili kwa vinara Benfica baada ya mechi tatu kucheza. Washambuliaji Bruno Cesar na Oscar Cardozo walifunga na kuendeleza rekodi ya ushindi ya klabu hiyo ya Ureno na kuvunja mwiko wa kocha wa Basel,Heiko Vogel wa kutofungwa nyumbani. Jijini Manchester, City walilazimika kusawazisha kabla ya kuichapa Villarreal wakati Aguero alipounganisha vizuri krosi ya Muargetina mwenzake Pablo Zabaleta kwa kuugusa kidogo na mpira kujaa wavuni dakika nne kabla ya filimbi ya mwisho. Cani alifunga bao la kuongoza kwa Villarreal katika dakika ya nne kwenye Uwanja wa Etihad, lakini City walisawazisha kupitia Carlos Marchena aliyejifunga mwenyewe dakika ya 43. Kocha wa Manchester City, Roberto Mancini alisema: “Nilisema kabla ya mchezo ni muhimu kwetu kushinda na nafikiri tulistahili kwa sababu tulitegeneza nafasi nyingi za kufunga. Lakini Villarreal ni timu nzuri kwenye mashambulizi ya kushitukiza kwa sababu wanacheza soka vizuri. “Unapocheza Ligi ya Mabingwa kwa mara ya kwanza kuna mengi ya kujifunza kila baada ya mchezo. Tunahitaji kushindi na firiki baada ya ushindi huu sasa tutafanya vizuri zaidi.” City sasa wameshika nafasi ya pili sawa na Napoli baada ya klabu hiyo ya Serie A kutoka sare na mabingwa mara nne Bayern Munich. Toni Kroos alifunga bao la kwanza kwa Bayern baada ya mabeki wa Napoli kufanya uzembe na kujisahau kumkaba katika dakika ya pili. Napoli ilisawazisha dakika ya 39 wakati beki wa Bayern, Holger Badstuber diverted in a cross from Christian Maggio. Kipa wa Napoli, Morgan De Sanctis alidaka penalti dhaifu iliyopigwa na Gomez dakika ya 49. Benzema alianza kwenye kikosi cha Madrid kilichokuwa kwenye kiwango cha juu. Benzema alifunga bao la kwanza akimalizia mpira wa kona uliopigwa na Oezil dakika ya 19, alitegeneza bao la pili kwa Khedira dakika ya 47 kabla ya Oezil kupachika bao la tatu kwa shuti lililopita katikati ya miguu ya kipa Hugo Lloris dakika ya 55, naye Sergi Ramos alipachika bao la nne akipokea kona ya Kaka.