Vigogo Man City waanza mikakati kwa Erling Haaland

New Content Item (1)

Muktasari:

  • Man City inataka kumsainisha mkataba mpya fundi huyu baada ya kuona timu mbalimbali zinaanza kuimendea huduma yake.

MABOSI wa Manchester City wamewekeza nguvu na akili zao kwenye mchakato wa kumsainisha mkataba mpya mshambuliaji wao kutoka Norway, Erling Haaland, 23, katika  dirisha hili.

Man City inataka kumsainisha mkataba mpya fundi huyu baada ya kuona timu mbalimbali zinaanza kuimendea huduma yake.

Haaland ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2027, msimu uliomalizika alicheza mechi 42 za michuano yote na kufunga mabao 38.

Mkataba mpya ambao Man City inamshawishi Haaland asaini unaweza ukamfanya kuwa mchezaji anayelipwa zaidi barani Ulaya.

Mara kadhaa Real Madrid imekuwa ikitajwa kuwa na mpango wa kumsajili ingawa kuna tetesi pia PSG inaweza kuwasilisha ofa kwa ajili ya kumchukua ili akazibe pengo la Kylian Mbappe.