Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Van Persie apambana Sterling aanze kucheza

VAN Pict

Muktasari:

  • Mkataba wa Sterling ni wa hadi mwisho wa msimu huu, lakini bado kuna matumaini kuwa unaweza kuongezwa kwa muda mrefu zaidi.

AMSTERDAM, UHOLANZI: WINGA machachari, Raheem Sterling amekamilisha uhamisho kwenda Feyenoord baada ya kuvunjwa kwa makubaliano ya pande zote mbili za mkataba wake na Chelsea katika dirisha la Januari, ambapo mchezaji huyo wa kimataifa wa England ameungana na Robin Van Persie.

Van Persie amethibitisha kuwa Feyenoord wameandaa haraka kambi ya mazoezi nchini Ubelgiji ili Sterling aweze kujiunga na wachezaji wenzake wapya.

Mchezaji huyo wa England alikamilisha kwa mshangao uhamisho kwenda klabu hiyo kubwa ya Uholanzi mapema wiki hii, baada ya kukubaliana kuvunja mkataba wake na Chelsea.

Inaelezwa kuwa Sterling alizungumza na klabu 18 kabla ya kuamua kujiunga na Feyenoord, ambako atacheza chini ya mshambuliaji wa zamani wa Arsenal na Manchester United, Van Persie.

Sterling hakuwa amecheza hata dakika moja kwa Chelsea msimu huu na ana hamu kubwa ya kuanza kwa kasi ili kufufua upya taaluma yake iliyokuwa ikisuasua. Hata hivyo, mchezaji huyo mwenye miaka 31 analazimika kusubiri kutokana na masuala ya kibali cha kazi.

Feyenoord ilicheza bila usajili wao huyo huru siku ya Jumapili, iliposhinda 1-0 dhidi ya Go Ahead Eagles, huku Sterling akiwa hawezi hata kufanya mazoezi na wachezaji wenzake wapya.

Lakini, ili kutatua tatizo hilo la muda, Van Persie amethibitisha kuwa wachezaji wake watasafiri kwa ajili ya kambi siku ya Jumatatu, ambako wataungana na Sterling, ambaye ni bingwa mara nne wa Ligi Kuu England.

Van Persie amesema: “Hilo linaruhusiwa nje ya nchi. Tunafanya kwa ajili yake, lakini pia nataka kufanyia kazi maendeleo ya timu yetu. Tunaweza kuwa na mazungumzo mazuri na kufanya jambo la kufurahisha pamoja.

"Ataanza mazoezi keshokutwa," aliongeza Van Persie. "Tutaangalia kila wiki kuona ni lini atakuwa tayari kwa mechi. Hilo litachukua muda, na hilo ni jambo la kawaida kwangu, kwa sababu hajacheza kwa miezi sita."

Akizungumza baada ya uhamisho wake kukamilika rasmi, Sterling amesema: "Kama mchezaji huru, nimepata kwa mara ya kwanza baada ya muda mrefu nafasi ya kudhibiti hatua inayofuata katika taaluma yangu. Nilitaka kuchukua muda kuzungumza na klabu na makocha wao wakuu ili kuelewa vizuri nafasi wanayonipangia na kuhakikisha ninaweza kuongeza thamani halisi katika sura hii mpya ya maisha yangu ya soka."

Mkataba wa Sterling ni wa hadi mwisho wa msimu huu, lakini bado kuna matumaini kuwa unaweza kuongezwa kwa muda mrefu zaidi.