Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Raheem Sterling anahitaji simu moja tu!

STERLING Pict

Muktasari:

  • Raheem Sterling amekuwa mchezaji maarufu zaidi kuachwa huru mwezi uliopita baada ya kufikia makubaliano ya pande zote na Chelsea kuvunja mkataba wake.

LONDON, ENGLAND: DIRISHA la usajili linafungwa leo, lakini bado kuna wachezaji wenye ubora mkubwa wanaopatikana kusajiliwa bila ada katika soko la uhamisho wa wachezaji huru na kinachotakiwa ni simu yako tu, waendee hewani.

Raheem Sterling amekuwa mchezaji maarufu zaidi kuachwa huru mwezi uliopita baada ya kufikia makubaliano ya pande zote na Chelsea kuvunja mkataba wake.

Kumekuwa na tetesi nyingi kuhusu hatima ya winga huyo, huku Fulham, West Ham United na Napoli zikitajwa kuwania saini yake.

Nyota huyo mwenye mechi 82 za kimataifa katika kikosi cha England si mchezaji pekee wa taifa hilo anayepatikana, kwani nyota wa zamani wa Manchester United, Jesse Lingard, aliachana na klabu ya Korea Kusini, FC Seoul, Desemba mwaka jana, hivyo simu moja tu, huduma yake inapatikana.

STER 01

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 huenda asikae muda mrefu bila klabu, baada ya kuhusishwa na uwezekano wa kuhamia Serie A ya Italia.

Ripoti pia zinasema amekuwa kwenye mazungumzo na klabu mbalimbali za Uingereza, zikiwemo baadhi za Ligi Kuu England. Mwenzake Lingard katika timu ya England hata kwenye kikosi cha Kombe la Dunia 2018, Dele Alli, bado hana klabu baada ya kuondoka Como mwaka jana.

Wakati huohuo, siku ya mwisho ya usajili ilipata msisimko baada ya taarifa Alex Oxlade-Chamberlain angepewa mkataba na Arsenal.

Kiungo huyo, aliyewahi kuichezea Arsenal kati ya mwaka 2011 na 2017, amekuwa akifanya mazoezi na kikosi cha vijana cha chini ya miaka 21.

Alipoulizwa kuhusu uwezekano wa kumsajili Oxlade-Chamberlain, Mikel Arteta amesema: “Tunachunguza kila chaguo.”

STER 02

Oxlade-Chamberlain bado yupo huru, pamoja na nyota wengine wa zamani wa kimataifa na Ligi Kuu England kama James Rodríguez, Divock Origi na Serge Aurier.

Gwiji wa zamani wa Hispania na Real Madrid, Sergio Ramos, pia hana klabu na bado hayuko tayari kustaafu akiwa na umri wa miaka 39, baada ya klabu yake ya mwisho kuwa Monterrey ya Mexico.

Beki huyo kwa sasa yuko bize kujaribu kuinunua klabu aliyoanzia soka lake, Sevilla, lakini bado hajastaafu rasmi.

Wachezaji wengine walio huru wanaopatikana ni pamoja na beki wa zamani wa Chelsea na West Ham, Kurt Zouma, pamoja na kipa Sergio Romero aliyewahi kuichezea Manchester United na beki wa kushoto wa zamani wa PSG, Juan Bernat.

Jumla ya Pauni 400 milioni zilitumika na klabu za Ligi Kuu England dirisha la usajili la Januari 2026.

Crystal Palace iliongoza kwa matumizi hayo baada ya kumsajili mshambuliaji wa Wolves, Jorgen Strand Larsen, kwa Pauni 48 milioni siku ya mwisho ya usajili.

STER 03
STER 03

Nyota wa zamani wa England, Kalvin Phillips, alipata klabu mpya baada ya kujiunga na Sheffield United kwa mkopo kutoka Man City.

Everton ilithibitisha kumsajili Tyrique George kwa mkopo kutoka Chelsea, huku Arsenal na Tottenham wakisajili vipaji vya akademi Evan Mooney na James Wilson mtawalia.