Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Raheem Sterling apata timu Uholanzi

STERLING Pict

Muktasari:

  • Klabu kadhaa zilionyesha nia mara tu mchezaji huyo wa kimataifa wa England mwenye mechi 82 alipokuwa mchezaji huru. Everton ilifanya mazungumzo kuhusu kunasa saini yake pamoja na Juventus na Napoli.

LONDON, ENGLAND: STAA, Raheem Sterling amekubali kujiunga na klabu ya Feyenoord ya Uholanzi hadi mwisho wa msimu.

Winga huyo alimaliza mgogoro wake na Chelsea mwezi uliopita baada ya kukubaliana na klabu hiyo kuvunja mkataba wake wenye thamani ya Pauni 325,000 kwa wiki aliokuwa nao kwenye kikosi hicho cha Stamford Bridge.

Klabu kadhaa zilionyesha nia mara tu mchezaji huyo wa kimataifa wa England mwenye mechi 82 alipokuwa mchezaji huru. Everton ilifanya mazungumzo kuhusu kunasa saini yake pamoja na Juventus na Napoli.

Inaelezwa kuwa Everton ilikuwa na nia kubwa zaidi kuliko klabu nyingine yoyote ya Ligi Kuu England, huku Leeds United pia ikifikiria uwezekano wa kumsajili. West Ham United iliwasiliana na Chelsea kuhusu uwezekano wa mkopo kwa Sterling kabla hajaafikiana kuondoka rasmi.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 alikutana na klabu na makocha kadhaa baada ya kuondoka Chelsea kabla ya kufanya uamuzi wa mwisho. Baada ya mazungumzo hayo, amechagua mkataba wa muda mfupi mjini Rotterdam baada ya kukutana na kocha wa Feyenoord, Robin van Persie. Straika huyo wa zamani wa Arsenal na Manchester United alikuwa mtu muhimu katika kumshawishi Sterling kujiunga na Eredivisie, huku Feyenoord ikimpa mkataba wa muda mfupi ili kufanya dili hilo livutie zaidi.

Awali klabu hiyo ya Uholanzi ilitoa mkataba wa muda mrefu, lakini Sterling amesaini hadi mwisho wa msimu ili kujiridhisha kuwa ni mahali sahihi kabla ya kujifunga kwa muda mrefu zaidi. Feyenoord iko nafasi ya pili kwenye msimamo wa Eredivisie na inapigania nafasi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, ingawa tayari wametolewa kwenye mashindano ya Ulaya msimu huu baada ya kumaliza nafasi ya 29 kwenye hatua ya makundi.

Sterling hakuwa amecheza mechi ya ushindani kwa Chelsea tangu Mei 2024 na alipitia kipindi kigumu alipokuwa kwa mkopo Arsenal msimu uliopita.

Winga huyo alikuwa akifanya mazoezi peke yake katika kituo cha mazoezi cha Chelsea cha Cobham baada ya kuwa sehemu ya kikosi kilichotengwa chini ya kocha wa zamani Enzo Maresca. Sterling alikuwa usajili wa kwanza chini ya umiliki wa sasa wa Wamarekani akijiunga kwa ada ya Pauni 47.5 milioni kutoka Manchester City, ambako alishinda mataji manne ya Ligi Kuu England.