Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Van Nistelrooy washamchoka

VAN Pict

Muktasari:

  • Leicester City imekuwa timu ya kwanza kwenye Ligi Kuu England kupoteza mechi sita mfululizo kwenye uwanja wa nyumbani huku ikishindwa kufunga bao lolote katika mechi hizo.

LEICESTER, ENGLAND: MASHABIKI wa Leicester City wameanza kumchoka kocha Ruud van Nistelrooy wakimtaka aondoke haraka baada ya kuona matokeo ya hovyo hayaonekani kukoma kwenye kikosi hicho.

Leicester City imekuwa timu ya kwanza kwenye Ligi Kuu England kupoteza mechi sita mfululizo kwenye uwanja wa nyumbani huku ikishindwa kufunga bao lolote katika mechi hizo.

Hilo limekuja baada ya Ijumaa iliyopita kukumbana na kichapo cha mabao 4-0 kutoka kwa Brentford uwanjani King Power, shukrani kwa mabao ya Yoane Wissa, Kevin Mbeumo, Christian Norgaard na Fabio Carvalho.

Kitu kibaya zaidi kwa Leicester City ni kwamba vipigo vyao sita vilivyopita, kikosi hicho cha kocha Van Nistelrooy kimeshindwa kufunga hata bao moja ili mashabiki wao walau wapate cha kushangilia.

Mabao yao ya mwisho kwenye Ligi Kuu England waliyofunga uwanjani King Power ilikuwa kwenye sare ya 2-2 dhidi ya Brighton, Desemba mwaka jana.

Katika mechi zao sita zilizopita, wamechapwa 3-0 na Wolves, 2-0 na Man City, 2-0 na Crystal Palace, 2-0 na Fulham, 2-0 na Arsenal na Ijumaa iliyopita ilichapwa 4-0 na Brentford.

Hiyo ina maana imeruhusu mabao 15 kwenye nyavu zao katika mechi hizo sita, huku yenyewe ikishindwa kufunga hata mara moja. Jambo hilo limewafanya kushika nafasi ya 19 kwenye msimamo wa Ligi Kuu England, huku ikiwa imeruhusu mabao 59 kwenye ligi hiyo hadi sasa.

Mashabiki wamechoka na matokeo hayo kwa sababu ukiweka kando vichapo hadi mabao hawafungi na shabiki mmoja alisema: "Aondoke." Shabiki mwingine alisema timu imekosa umoja na kudai Van Nistelrooy afukuzwe.

MECHI ZIJAZO

ZA LECESTER

-Februari 27 vs West Ham (ugenini)

-Machi 9 vs Chelsea (ugenini)

-Machi 16 vs Man United (nyumbani)

-Aprili 2 vs Man City (ugenini)

-Aprili 5 vs Newcastle (nyumbani)

-Aprili 12 vs Brighton (ugenini)