Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Van Dijk ajifikiria upya hatima yake

Muktasari:

  • Van Dijk, 34, anaona kasi ya mchezo sasa inaanza kumtupa mkono, lakini wachezaji wengi wamecheza soka kwa muda mrefu kwenye klabu zao baada ya kutangaza kutundika daruga kwenye soka la kimataifa.

LIVERPOOL, ENGLAND: BEKI wa kati wa Liverpool, Virgil van Dijk ameripotiwa atafikiria hatima ya soka lake baada ya kuiongoza Uholanzi kwenye fainali za Kombe la Dunia 2026.

Van Dijk, 34, anaona kasi ya mchezo sasa inaanza kumtupa mkono, lakini wachezaji wengi wamecheza soka kwa muda mrefu kwenye klabu zao baada ya kutangaza kutundika daruga kwenye soka la kimataifa.

Akizungumza baada ya Uholanzi kukamatia tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia 2026, Van Dijk alisema hizo zinaweza kuwa fainali zake kubwa za mwisho kuitumikia nchi yake.

Alisema: “Nataka kumshukuru kila mtu aliyepo hapa, wachezaji wote, maofisa wote na watu wote kwa kila kitu walichofanya huko nyuma ya pazia. Najivunia kuwa nahodha wa Oranje na kuwaongoza kwenye kila mechi. Nasubiria kwa hamu fainali zangu za mwisho na natamani kwenda kupata mafanikio pamoja.”

Zilikuwa mbio za farasi wawili kwenye Kundi G la mechi za kufuzu Kombe la Dunia, ambapo Poland ilikuwa mpinzani mkubwa wa Uholanzi katika msako wa tiketi hiyo ya kwenda kwenye fainali hizo zitakazofanyika mwakani huko Marekani, Canada na Mexico.

Lakini, kikosi hicho cha Uholanzi kinachonolewa na Ronald Koeman kilimaliza kileleni kwa tofauti ya pointi tatu na kufuzu moja kwa moja kwa fainali hizo, ambapo haikupoteza mechi yoyote na kufunga mabao 27.

Van Dijk alionyesha kiwango bora msimu uliopita alipoiongoza Liverpool kushinda ubingwa wa Ligi Kuu England katika msimu wa kwanza wa kocha Arne Slot. Lakini, mambo yamekuwa magumu msimu huu baada ya kuanza vizuri, kisha kutibua mambo na timu sasa ilishuka kwenye msimamo wa ligi hadi nafasi ya nane, pointi nane nyuma ya vinara Arsenal.