Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Uongozi Man United kumrudisha nyumbani Solskjaer

OLE Pict

Muktasari:

  • Man United imeripotiwa kuzungumza na staa wa zamani wa timu hiyo, ambaye pia aliwahi kuwa kocha wa muda kwenye kikosi hicho cha Old Trafford, Michael Carrick, ambaye aliongoza timu hiyo kwenye mechi tatu na haijapoteza hata moja mwaka 2021.

MANCHESTER, ENGLAND: MAMBO ni moto. Manchester United imemweka kwenye orodha Ole Gunnar Solskjaer ikitaka kumrudisha kuwa kocha wa muda kwa mara ya pili katika kikosi hicho chenye maskani yake Old Trafford.

Solskjaer, ambaye alikuwa kocha wa muda wa Man United na kuinoa katika mechi 17 msimu wa 2018-19 kabla hajakabidhiwa mikoba hiyo jumla, kwa sasa anaripotiwa kuwa namba moja katika orodha ya wanaohusishwa kwenye kuchukua mikoba ya kuinoa timu hiyo hadi mwisho wa msimu baada ya Ruben Amorim kufutwa kazi Jumatatu iliyopita.

Man United imeripotiwa kuzungumza na staa wa zamani wa timu hiyo, ambaye pia aliwahi kuwa kocha wa muda kwenye kikosi hicho cha Old Trafford, Michael Carrick, ambaye aliongoza timu hiyo kwenye mechi tatu na haijapoteza hata moja mwaka 2021.

Solskjaer aliinoa Man United kati ya Desemba 2018 na Novemba 2021, wakati alipofutwa kazi baada ya vichapo vitano katika mechi saba za Ligi Kuu England, huku kipigo cha mwisho ni kile cha 5-0 kutoka kwa Liverpool.

Solskjaer, 52, alirejea Manchester, Septemba mwaka jana baada ya kufutwa kazi Besiktas na alipata fursa ya kukutana na wachezaji wenzake wa zamani waliocheza pamoja Old Trafford. Darren Fletcher amechukua mikoba ya kuinoa Man United kwa muda, akiongoza timu hiyo katika mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Burnley, usiku wa Jumatano na anajiandaa kwa mazungumzo juu ya nafasi hiyo baada ya mechi.

Fletcher alirudi Man United wakati Solskjaer alipokuwa kocha Januari 2021, ambapo awali alikuwa sehemu ya benchi la ufundi la kikosi cha kwanza.

Man United baadaye ilimpa Fletcher nafasi ya kuwa kocha wa mpito, lakini bado haijawekwa wazi kama ataendelea kuinoa timu hiyo baada ya mechi ya Turf Moor. Akizungumza juu ya nafasi ya kuwa kocha wa kudumu, Fletcher amesema: “Ukweli, si kitu ambacho nilikitarajia kabisa. Niliwekeza akili yangu kwenye mechi ya Burnley. Nadhani huo ni mjadala unaopaswa kuendelea baada ya mechi. Kama nilivyosema, kuna mambo mengi yalikuwa yakiendelea.”

Alipoulizwa kuhusu kuinoa Man United, Fletcher aliongeza: “Hii ni heshima. Naweza kusema ni heshima kubwa, nawaza juu ya kuiongoza Manchester United. Sikuwahi kuwa na hiyo ndoto kwamba kuna siku moja hicho kitu kitakuja kutokea. Lakini, kuiongoza timu hiyo ni heshima kubwa na najivunia kwa hilo. Kila kitu kimetokea kwa haraka. Kulikuwa na mechi, ilibidi tufanye mazoezi na nimezungumza na wachezaji.”

Rekodi za Ole Gunnar Solskjaer kwenye kikosi cha Man United ni kwamba alikiongoza katika mechi 91 za ushindi, sare 37 na vichapo 40.


MECHI ZIJAZO ZA MAN UNITED

-Januari 11 vs Brighton (nyumbani)

-Januari 17 vs Man City (nyumbani)

-Januari 25 vs Arsenal (ugenini)

-Februari 1 vs Fulham (nyumbani)

-Februari 7 vs Tottenham (nyumbani)

-Februari 10 vs West Ham (ugenini)

-Februari 23 vs Everton (ugenini)

-Februari 28 vs Crystal Palace (nyumbani)