Una hela? Hilo swali haliwahusu hawa jamaa
Muktasari:
- Pesa nyingi sana zitatumika kwenye soka la kisasa, wanasoka wakivunja vibunda vya maana kupitia mishahara yao, bonasi na dili nyingine za matangazo ya kibiashara.
LONDON, ENGLAND: UNA hela? Si unajua tena, siku hizi hapendwi mtu, linapendwa pochi.
Lakini, swali hilo usimuulize mwanasoka anayetamba kwenye Ligi Kuu za Ulaya. Hao watu wana mkwanja mrefu si kitoto.
Pesa nyingi sana zitatumika kwenye soka la kisasa, wanasoka wakivunja vibunda vya maana kupitia mishahara yao, bonasi na dili nyingine za matangazo ya kibiashara.
Na kitu kinachovutia zaidi, hiyo mikwanja wanayovuna, inalipwa kwa wiki. Sawa kuna mastaa kama Cristiano Ronaldo na Karim Benzema wanaolipwa pesa nyingi huko Saudi Pro League, lakini kuna wakali wengi sana wanalipwa vizuri kwa wanaocheza soka kwenye ligi za Ulaya.
Habari ndio hiyo kwenye Ligi Kuu tano bora za Ulaya, ambzo ni Premier League, La Liga, Serie A, Bundesliga na Ligue 1. Miamba ya soka kama Real Madrid, Paris Saint-Germain, Manchester City na Manchester United imekuwa ikilipa wachezaji wake mishahara mitamu sana.
Katika kuthibitisha hilo, hii hapa orodha ya masupastaa 25 wa soka la Ulaya ambao wamekuwa wakilipwa mishahara mikubwa kwa kila wiki kwa mujibu wa takwimu za mtandao wa Capology.
Kwenye orodha hiyo mchezaji anayelipwa mshahara mdogo ni yule anayepokea Pauni 250,000 kwa wiki, ambayo ni zaidi ya Sh816milioni kwa pesa ya Kitanzania, ambayo kila wiki inaingia kwenye akaunti ya benki yake.
25.Lautaro Martinez (Inter)
Mshahara: Pauni 276,395 kwa wiki
24.Alexander Isak (Liverpool)
Mshahara: Pauni 280,000 kwa wiki
23.Kai Havertz (Arsenal)
Mshahara: Pauni 280,000 kwa wiki
22.Omar Marmoush (Manchester City)
Mshahara: Pauni 295,000 kwa wiki
21.Ousmane Dembele (PSG)
Mshahara: Pauni 298,447 kwa wiki
20.Bernardo Silva (Man City)
Mshahara: Pauni 300,000 kwa wiki
19.Bruno Fernandes (Man United)
Mshahara: Pauni 300,000 kwa wiki
18.Serge Gnabry (Bayern Munich)
Mshahara: Pauni 312,872 kwa wiki
17.Jamal Musiala (Bayern Munich)
Mshahara: Pauni 312,872 kwa wiki
16.Frenkie de Jong (Barcelona)
Mshahara: Pauni 315,027 kwa wiki
15.Raheem Sterling (Chelsea)
Mshahara: Pauni 325,000 kwa wiki
14.Joshua Kimmich (Bayern Munich)
Mshahara: Pauni 331,607 kwa wiki
13.Jan Oblak (Atletico Madrid)
Mshahara: £345,369 kwa wiki
12.Vinicius Junior (Real Madrid)
Mshahara: Pauni 345,369 kwa wiki
11.Jude Bellingham (Real Madrid)
Mshahara: Pauni 345,369 kwa wiki
10.Robert Lewandowski (Barcelona)
Mshahara: Pauni 345,369 kwa wiki
9.Manuel Neuer (Bayern Munich)
Mshahara: Pauni 348,188 kwa wiki
8.Virgil van Dijk (Liverpool)
Mshahara: Pauni 350,000 kwa wiki
7.Casemiro (Man United)
Mshahara: Pauni 350,000 kwa wiki
6.Dusan Vlahovic (Juventus)
Mshahara: Pauni 368,416 ka wiki
5.David Alaba (Real Madrid)
Mshahara: Pauni 373,058 kwa wiki
4.Mohamed Salah (Liverpool)
Mshahara: Pauni 400,000 kwa wiki
3.Harry Kane (Bayern Munich)
Mshahara: Pauni 414,509 kwa wiki
2.Kylian Mbappe (Real Madrid)
Mshahara: Pauni 518,137 kwa wiki
1.Erling Haaland (Man City)
Mshahara: Pauni 525,000 kwa wiki