Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Henderson anajuta kuondoka Liverpool, afunguka yaliyomsibu Saudia

HERNDERSON Pict

Muktasari:

  • kiungo huyo, ambaye anatarajiwa kuichezea England kwa mara ya 86 dhidi ya Wales katika mechi ya kirafiki kwenye uwanja wa Wembley Oktoba 9, 2025, anasema ana majeraha ya kiakili kutokana na nyakati ngumu alizopitia kwenye maisha yake ya soka, japo baadhi ya matatizo alijisababishia mwenyewe.

Huenda kiungo Jordan Henderson akawa sehemu ya kikosi cha England kitakachoshiriki fainali za Kombe la Dunia 2026 chini ya kocha Thomas Tuchel, kufuatia kiwango bora anachoendelea kukionyesha akiwa na klabu ya Brentford inayoshiriki Ligi Kuu ya England.

kiungo huyo, ambaye anatarajiwa kuichezea England kwa mara ya 86 dhidi ya Wales katika mechi ya kirafiki kwenye uwanja wa Wembley Oktoba 9, 2025, anasema ana majeraha ya kiakili kutokana na nyakati ngumu alizopitia kwenye maisha yake ya soka, japo baadhi ya matatizo alijisababishia mwenyewe.

Henderson, mwenye umri wa miaka 35, amezungumza kwa mara ya kwanza kwa kina kuhusu changamoto alizopitia baada ya kuondoka Liverpool, klabu aliyoitumikia kwa miaka 12.

Amekiri kuwa baada ya kuondoka Liverpool, hakuweza hata kuangalia mechi za timu yake ya zamani, huku akisisitiza kuwa huenda hilo likawafanya mashabiki wengi wakamcheka au kumuhurumia kidogo, hasa ikizingatiwa alikubali mshahara wa pauni 350,000 kwa wiki kuhamia Saudi Arabia kuichezea Al-Ettifaq.

Uamuzi huo ulikuwa janga kubwa la mawasiliano kwake na ndipo alipofanya uamuzi kuhamia Ajax kabla ya kurejea Ligi Kuu ya England na kutua Brentford.

HE 01

Henderson alikuwa katika hali nzuri alipoingia katika chumba cha waandishi wa habari kwenye kituo cha St George’s Park. Lakini alibadilika haraka na kuwa na hisia kali alipoulizwa kuhusu kuondoka kwake Liverpool mwaka 2023, klabu aliyoisaidia kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya na Ligi Kuu ya England.

Henderson amesema: “Ilikuwa kipindi kigumu sana kuondoka Liverpool. Nilikuwa pale kwa muda mrefu, miaka 12. Kuondoka Liverpool kulikuwa jambo kubwa na gumu sana. Ilikuwa sehemu ya maisha yangu kwa muda mrefu na ghafla ikawa imeisha hivyo.

"Nilipata wakati mgumu baada ya hapo. Nilikuwa nimejenga uhusiano wa karibu sana na nilijitolea maisha yangu huko. Sikuweza kuangalia mechi nyingi, hasa za Liverpool. Kwa hiyo pengine nilikuwa mahali sahihi, kwa sababu nilikuwa upande mwingine wa dunia!"

Uhamisho wake kwenda Mashariki ya Kati uliathiri sifa yake njema ya awali, na licha ya kuondoka Saudi Arabia kwenda Ajax Januari 2024, kocha wa zamani wa England, Gareth Southgate, hakumjumuisha kwenye kikosi cha Euro kutokana na kushuka kiwango.

HE 02

Henderson amesema: “Sidhani kama Saudi ndiyo sababu ya mimi kukosa fainali za Euro 2024. Nilipokuwa Saudi, nilikuwa kwenye kila kambi ya timu ya taifa kabla ya mashindano hayo.

"Kwa kutazama nyuma, labda ningefanya maamuzi tofauti. Lakini kwa wakati huo, ndivyo nilivyojisikia na ndivyo nilivyoamua kwa sababu mbalimbali.

"Nilijaribu kufanya jambo sahihi. Nilifikiri ilikuwa sahihi kwa wakati huo, na baadaye nikahisi kurudi Ulaya na kucheza Ajax ilikuwa sahihi pia na niliifurahia sana.

“Katika miaka michache iliyopita, nimepitia nyakati ngumu sana lakini unapovuka na kutoka upande mwingine, unajifunza mengi kukuhusu wewe mwenyewe na hiyo hukufanya kuwa imara zaidi.

"Bila shaka, mimi si mkamilifu na nimefanya makosa katika maisha yangu ya soka. Lakini kile ambacho nimejaribu kufanya kila wakati ni jambo sahihi, kuwasaidia watu walioko karibu yangu, na kutumia changamoto kunifanya kuwa mchezaji bora na kusaidia timu yangu popote nilipo. Nafikiri katika soka, kila wakati unapaswa kuthibitisha thamani yako. Ukifikiri huwezi tena kuthibitisha chochote, basi una tatizo. 

HE 03

"Katika maisha yangu yote ya soka, nimekuwa nikilazimika kuthibitisha uwezo wangu. Kwa hiyo hili halikuwa jipya. Nimejaribu tu kufanya kile kilicho bora kwa timu na kucheza kwa kiwango kizuri na kufurahia pia. Kucheza kila wiki kunasaidia sana katika hilo. Lakini kwa ujumla, nimefurahi sana mwanzo wangu na kufurahia kurudi Ligi Kuu na hilo limenipa nguvu mpya ya kutaka kuendelea kucheza katika ligi bora zaidi duniani.”