Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Umri ni namba tu, Kombe la Dunia 2026

MILLER Pict

Muktasari:

  • Leo, Jumanne kwa kuanzia tutatazama rekodi ya tofauti kubwa zaidi ya umri kuwahi kutokea kati ya wachezaji wawili wa timu moja katika Kombe la Dunia, rekodi iliyowekwa na wachezaji wa Cameroon katika Michuano ya mwaka 1994 nchini Marekani.

YAOUNDE, CAMEROON: WAKATI dunia ikisubiri kwa hamu kuanza kwa fainali za Kombe la Dunia 2026, Mwanaspoti linaendelea kuhesabu siku kuelekea mashindano hayo kwa kuangazia rekodi mbalimbali zilizowahi kuwekwa.

Leo, Jumanne kwa kuanzia tutatazama rekodi ya tofauti kubwa zaidi ya umri kuwahi kutokea kati ya wachezaji wawili wa timu moja katika Kombe la Dunia, rekodi iliyowekwa na wachezaji wa Cameroon katika Michuano ya mwaka 1994 nchini Marekani.

Katika fainali hizo za 1994, nyota mkongwe Roger Milla alikuwa na umri wa miaka 42 huku mchezaji kijana Rigobert Song akiwa na miaka 17 pekee. Tofauti hiyo ya miaka 24 na siku 42 ndiyo kubwa zaidi kuwahi kurekodiwa kati ya wachezaji wa timu moja katika historia ya Kombe la Dunia.

MILL 01

Milla pia aliweka historia kwa kuwa mchezaji wa kwanza wa nje ya nafasi ya kipa kucheza Kombe la Dunia akiwa na umri wa zaidi ya miaka 40, hatua iliyomfanya aendelee kuwa moja ya majina makubwa katika historia ya soka la Afrika.

Kwa upande wake, Song alikumbuka namna alivyoshtuka kuitwa katika kikosi hicho akiwa kijana mdogo sana mwenye ndoto kubwa.

“Nilikuwa siamini nilipoitwa kwenye kikosi. Nilikuwa nimetazama Kombe la Dunia la 1990 kupitia televisheni ndogo nyeusi na nyeupe huku nikimshangaa Roger Milla. Alileta furaha kubwa Cameroon,’’ amesema Song.

MILL 02

Aliongeza kuwa hakuwahi kufikiria kwamba miaka minne baadaye angekuwa akicheza pamoja na shujaa wake huyo katika Kombe la Dunia.

‘‘Haikuwa hata ndoto yangu kufikiria kwamba miaka minne baadaye ningekuwa mchezaji mwenzake kwenye Kombe la Dunia. Nilikuwa na miaka 17 tu na yeye alikuwa Roger Milla aliongeza.

Milla naye alieleza kuwa rekodi hiyo ni ushahidi wa nguvu ya vipaji vya Cameroon.

“Hii ni rekodi ninayojivunia. Tulionyesha kwamba Cameroon ni nchi yenye vipaji vingi na hakuna pengo kati ya vizazi”  amesema nyota huyo aliyepewa jina la ‘Simba Mzee’.

MILL 03

Katika Kombe la Dunia la 1994, Roger Milla aliendelea kuandika historia baada ya kufunga bao dhidi ya Russia akiwa na miaka 42 na kuwa mfungaji mwenye umri mkubwa zaidi kuwahi kufunga katika historia ya Kombe la Dunia hadi sasa.

Licha ya bao hilo, Cameroon ilipokea kichapo cha mabao 6-1 kutoka Russia katika mchezo ambao mshambuliaji Oleg Salenko aliweka rekodi ya kipekee kwa kufunga mabao matano katika mechi moja ya Kombe la Dunia.

Kadri siku zinavyosogea kuelekea Kombe la Dunia 2026, simulizi kama hizi zinaendelea kuonyesha namna mashindano hayo yalivyojaa historia, rekodi na hadithi zisizosahaulika katika ulimwengu wa soka.