Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Umesikia hii ya Vinicius Jr, mashabiki Real Madrid wahusishwa

VINI Pict

Muktasari:

  • Moja ya malengo makuu ya Liverpool mwaka huu ni kumsajili winga. Ingawa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu England bado wanaye Mohamed Salah kikosini, nia yao ya awali kwa Antoine Semenyo kabla ya winga huyo wa kimataifa wa Ghana kujiunga na Manchester City inaonyesha wazi dhamira yao ya kuleta mchezaji wa kiwango cha juu pembeni.

LIVERPOOL, ENGLAND: NDO hivyo. Liverpool imepata msukumo mkubwa katika juhudi zao za kumleta nyota wa Real Madrid, Vinicius Junior kwenda Anfield mwaka huu, baada ya ripoti kadhaa kutoka vyombo vya habari vya Hispania kudai mchezaji huyo alivunjika moyo na kulia baada ya kuzomewa na mashabiki wa Estadio Bernabeu.

Moja ya malengo makuu ya Liverpool mwaka huu ni kumsajili winga. Ingawa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu England bado wanaye Mohamed Salah kikosini, nia yao ya awali kwa Antoine Semenyo kabla ya winga huyo wa kimataifa wa Ghana kujiunga na Manchester City inaonyesha wazi dhamira yao ya kuleta mchezaji wa kiwango cha juu pembeni.

Miongoni mwa mawinga wengi wanaofuatiliwa kwa karibu na Liverpool ni nyota wa Real Madrid, Vinícius Jr.

Mtaalamu wa masuala ya usajili, Graeme Bailey, aliripoti Desemba 22 mwaka jana kuwa Liverpool ni miongoni mwa klabu zinazovutiwa na dili la Vinícius Jr.

VIN 01

Chelsea na Manchester City pia zina nia kubwa kwa winga huyo, huku vyanzo vikidai mawakala wanaofanya kazi na Vinícius Jr wameziarifu Liverpool, Chelsea na Man City kuwa mchezaji huyo ana nia ya kuhamia England.

Vinícius Jr ana mkataba Real Madrid hadi majira ya joto ya 2027, lakini mazungumzo ya mkataba mpya yamesitishwa kutokana na kutoridhika kwake chini ya kocha Xabi Alonso, ambaye alifutwa kazi na klabu hiyo wiki iliyopita na nafasi yake kuchukuliwa na Alvaro Arbeloa.

Ingawa Vinícius Jr huenda alifurahia kuondoka kwa Alonso, ambaye aligombana naye wakati wa El Clásico dhidi ya Barcelona mapema msimu huu, mashabiki wa Estadio Bernabéu hawaridhishwi naye. Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Hispania, mashabiki wa Madrid walimzomea Vinícius Jr wakati wa mazoezi ya kabla ya mechi na pia wakati jina lake lilipotangazwa kama mchezaji wa kikosi cha kwanza kabla ya mechi dhidi ya Levante, Jumamosi iliyopita.

VIN 02

Cadena SER ilichapisha kipande cha video kwenye tovuti yake kikimuonyesha Vinícius Jr “akilia baada ya kutambua ukubwa wa makelele ya kuzomewa aliyopata kabla ya mechi.”

Gazeti la AS, linaloegemea upande wa Real Madrid, liliripoti kuwa mashabiki wa Madrid walikuwa wakimzomea Vinícius Jr kila alipogusa mpira.

“Kuzomewa kwa Vinícius na mashabiki wa Madrid kulikuwa wazi na bila shaka,” ilisema ripoti hiyo, ikiongeza mchezaji huyo wa Brazil alikuwa amevunjika moyo kiasi kwamba baada ya jina lake kuzomewa kupitia mfumo wa matangazo kabla ya mechi, mwenzake Kylian Mbappé alilazimika kwenda kumfariji.

Gazeti la Marca, nalo likiripoti kutoka mtazamo wa Real Madrid, lilidai kuzomewa huko kulitokana na mashabiki “kumtaja wazi Vinícius kama mmoja wa waliohusika na kuondoka kwa Xabi Alonso jambo ambalo mashabiki hawasamehi.”

Ripoti hiyo iliongeza: “Mbrazili huyo amekuwa akifuatiliwa kwa karibu kwa wiki kadhaa kutokana na mwenendo wake uwanjani. Kuzomewa kulikokuwa kunazidi kuongezeka tayari kulikuwa kumemsindikiza katika mechi zilizopita, lakini dhidi ya Levante hali ilifikia hatua ya kilele.”

Real Madrid ilishinda 2-0 dhidi ya Levante, lakini licha ya ushindi huo, mashabiki hawakuridhishwa na kiwango cha uchezaji na Vinícius Jr aliondoka uwanjani bila kuwashukuru mashabiki.

VIN 03

Marca ilibaini: “Mara tu mwamuzi alipopuliza filimbi ya mwisho, Vinícius alikimbia moja kwa moja kuelekea vyumba vya kubadilishia nguo bila kumtazama au kumshukuru mtu yeyote. Kitendo hiki kinaashiria wakati mgumu katika uhusiano wake na mashabiki na kinaweza kuwa mwanzo wa mabadiliko makubwa katika safari yake na Real Madrid.”

Hali ya Vinícius Jr akiwa na Real Madrid kwa sasa imefikia kiwango cha chini kabisa na hilo linafungua mlango kwa Liverpool kuingilia kati.

Vyanzo vimeeleza kuwa Madrid hawako tayari kumuuza Vinícius Jr dirisha la usajili la Januari, lakini uhamisho kwenda Liverpool katika majira ya joto ya 2026 unawezekana, hasa iwapo mchezaji huyo atashindwa kuinua kiwango chake.

Mashabiki wa Real Madrid hawasamehi, na hapo awali wamewahi kuwazomea wachezaji wakubwa kama Cristiano Ronaldo, Gareth Bale, Zinedine Zidane na Alfredo Di Stéfano.

Funguo la mustakabali wa muda mrefu wa Vinícius Jr Madrid ni namna atakavyoitikia presha ya kuzomewa na mluzi wa mashabiki.

Iwapo atashindwa kustahimili presha na akaendelea kuwa nje ya kiwango hadi mwisho wa msimu, kutokana na hali ya mkataba wake, Madrid huenda wasiwe na pingamizi la kumuuza.

Na Liverpool watakuwa tayari kuchukua fursa hiyo.