Ulaya yote mambo ni motomoto

Muktasari:
- Ni mechi za kibabe, huku Bayern ikitegemea huduma ya straika wao Harry Kane ili kutimiza lengo lao la kuwapoka Leverkusen taji hilo.
MUNICH, UJERUMANI: BALAA hilo. Ndicho unachoweza kusema wakati vita ya kusaka ubingwa wa Bundesliga utakapoendelea, ambapo Bayern Munich na Bayer Leverkusen zitakuwa nyumbani kukipiga na vfL Bochum na Werder Bremen mtawalia, Jumamosi.
Ni mechi za kibabe, huku Bayern ikitegemea huduma ya straika wao Harry Kane ili kutimiza lengo lao la kuwapoka Leverkusen taji hilo.
Borussia Dortmund nayo itakuwa nyumbani kucheza na Augsburg, Holstein Kiel na VfB Stuttgart, Wolfsburg na St.Pauli na Freiburg na RB Leipzig.
Jumapili kutakuwa na mechi mbili, Eintracht Frankfurt itacheza na Union Berlin na Hoffenheim itacheza na FC Heidenheim.
Kwenye La Liga, Celta Vigo itacheza na Leganes, Alaves na Villarreal, Valencia na Real Valladolid, wakati Barcelona itakipiga na Osasuna Jumamosi, kabla ya Jumapili, Getafe kucheza na Atletico Madrid, Real Madrid na Rayo Vallecano, Athletic Bilbao na Mallorca, Real Betis na Las Palmas na Real Sociedad na Sevilla.
Kwenye Ligue 1, Rennes itakuwa nyumbani kucheza na PSG, Lille na Montpellier na mechi ya mwisho kwa Jumamosi ni Marseille na Lens, huku Jumapili kitapigwa kipute cha Brest na Angers, Le Havre na Saint-Etienne, Nantes na Strasbourg na Nice itacheza na Lyon.
Huko Serie A, habari ni kipute cha Parma na Torino, Como 1907 na Venezia, Lecce na AC Milan na Inter Milan na Monza itamaliza siku kwa mechi za Jumapili, huku kwa Jumapili, Hellas Verona na Bologna, Napoli na Fiorentina, Empoli na AS Roma, wakati Juventus itamaliza ubishi na Atalata. Mambo ni moto.