Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Uganda yabadili makipa watatu, lakini wapi!

UGANDA Pict

Muktasari:

  • The Cranes ilihitaji ushindi kwenye mechi hiyo ya mwisho ya makundi ili kusonga mbele kwenye Kundi C lililokuwa pia na timu za Nigeria, Tunisia na Tanzania, ambazo zote zimevuka.

MARRAKECH, MOROCCO: UGANDA imetupwa nje ya mashindano ya AFCON 2025 licha ya kutumia makipa wote watatu kwenye mechi yao ya Nigeria iliyomalizika kwa kichapo cha mabao 3-1.

The Cranes ilihitaji ushindi kwenye mechi hiyo ya mwisho ya makundi ili kusonga mbele kwenye Kundi C lililokuwa pia na timu za Nigeria, Tunisia na Tanzania, ambazo zote zimevuka.

Kwa Uganda hali ilikuwa mbaya, ikipoteza kwa mabao ya Raphael Onyedika, aliyefunga mara mbili na Paul Onuachu, aliyefunga la kwanza.

Uganda iliona dalili mapema kwamba mambo yanaweza kuwa magumu upande wao baada ya kumpoteza kipa Denis Onyango aliyejiumiza enka wakati alipokuwa akizuia mpira wa kona wakati matokeo yakiwa 0-0, ambapo kipa huyo mwenye umri wa miaka 40 alifanya sevu ya kibabe kumgomea straika wa zamani wa Southampton, Onuachu kuifungia bao Super Eagles.

Lakini, alimfunga kwenye dakika 28 wakati Onuachu alipomaliza ukame wake wa mabao wa miaka minne kwenye soka la kimataifa. Straika huyo wa Trabzonspor, ambaye alishuka daraja mara mbili akiwa na Southampton, aliunganisha nyavuni pasi ya kiungo wa zamani wa Sheffield Wednesday, Fisayo Dele-Bashiru.

Onyango alihitaji kutibuwa tena kabla ya mapumziko na nafasi yake ilichukuliwa na kipa Salim Magoola kwenye kipindi cha pili. Hata hivyo, Magoola alicheza kwa dakika 11 tu.

Kipa huyo alijaribu kumzuia Victor Osimhen asifunge kwa kutumia mikono kuzuia mpira nje ya boksi na hivyo kuonyeshwa kadi nyekundu.

Baada ya hapo, Uganda ililazimika kumwingiza kipa chaguo la tatu, Nafian Alionzi, ambaye alijikuta akiokota mpira kwenye nyavu zake dakika ya tatu tu tangu alipoingizwa. Staa wa Club Brugge, Onyedika alimpiga tobo kipa huyo na kufunga katika dakika 62 kabla ya kuifungia Nigeria bao la tatu dakika tano baadaye. Ushindi huo uliifanya Nigeria kutinga hatua ya 16 bora kwa kishindo, ikishinda mechi zote tatu kwenye Kundi C, huku katika mechi hiyo ya Uganda iliwapumzisha mastaa wake, Ademola Lookman, Alex Iwobi na Wilfred Ndidi.

Uganda ilipata bao lake la kujifariji kupitia kwa Rogers Mato baada ya kazi nzuri ya Allen Okello kwenye dakika 76, aliposukumia mpira nyavuni kwa ustadi akimshinda kipa Francis Uzoho.