Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ubingwa EPL ni 50 kwa 50

EPL Pict

Muktasari:

  • Kwa ujumla, raundi ya 34 inaonekana kuwa na ushindani mkubwa na inaweza kuwa na athari kubwa katika mbio za ubingwa, nafasi za kufuzu mashindano ya Ulaya na vita ya kushuka daraja, huku supercomputer ya Opta ikitoa mwanga wa kile kinachoweza kutokea, lakini matokeo halisi yataamuliwa uwanjani.

LONDON, ENGLAND: MSIMU wa 2025/26 unakaribia kufika mwisho, ambapo ni ligi moja tu kati ya tano bora Ulaya ambayo imeshapata bingwa, Ujerumani (Bundesliga). Bayern Munich imeshatangazwa bingwa kwa msimu mwingine ikiwa ni mara ya 35 kubeba ubingwa huo.

Lakini, vita inasonga katika ligi zingine na kwa England imekolea zaidi, lakini kwa mara nyingine, supercomputer ya Opta imeibuka tena na utabiri wake ikitoa makadirio yanayotegemea takwimu kwa mechi zote zilizobaki za Ligi Kuu England na matokeo ya msimu mzima, ambapo licha ya Manchester City kuwa kileleni mwa msimamo, lakini imeonyesha kwamba Arsenal ina uwezekano mkubwa wa kubeba ubingwa.

Kompyuta hiyo inayotumia akili bandia (AI), ilionyesha uwezo mkubwa wa kutabiri msimu wa 2024-25, na imeendelea kuvutia mashabiki wengi wa soka Ulaya katika msimu huu licha ya kuwapo kwa ushindani mkali, na kadri mwisho wa msimu unavyokaribia imetabiri kwamba Gunners inaweza isitoke kapa ikiipa nafasi kubwa ya kuondoka na mwali.

EP 01

Man City waliowafunga Arsenal wiki iliyopita walipanda kileleni mwa msimamo baada ya kuifunga Burnley, Jumatano, wiki hii ushindi uliowashusha Burnley hadi Championship. Wakati huohuo, Brighton waliizidishia matatizo Chelsea na kuipita kwenye msimamo, hali iliyosababisha kocha Liam Rosenior kutimuliwa.

Bournemouth waliipita Chelsea baada ya sare na Leeds United, ambao walipata bao la kusawazisha dakika za mwisho na hivyo kusogea karibu zaidi na kupona kutoka kushuka daraja. Sehemu iliyobaki ya raundi hii ya 35 itaendelea leo.

Aston Villa wanaweza kuimarisha nafasi ndani ya tano bora watakapokutana na Fulham leo, Jumamosi, ambapo Tottenham Hotspur watasafiri kucheza na Wolverhampton Wanderers wakisaka ushindi wa kwanza mwaka 2026, huku Liverpool wakitarajia kuendeleza mfululizo wa ushindi watakapoikaribisha Crystal Palace.

EP 02

Arsenal wana nafasi ya kurejea kileleni mwa msimamo ikiwa watashinda dhidi ya Newcastle United katika mchezo mwingine na raundi hiyo itahitimishwa keshokutwa, Jumatatu, kwa pambano kati ya Manchester United na Brentford.

Kwa mujibu wa utabiri wa Opta, Arsenal pia wana nafasi kubwa ya kushinda mwishoni mwa wiki hii, wakiwa na asilimia 68.4 ya ushindi dhidi ya Newcastle United leo. Pia, Manchester United, Aston Villa na Liverpool wanatarajiwa kupata ushindi ambao unaweza kuwasogeza zaidi kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya. Kompyuta hiyo pia inaipa nafasi Tottenham ushindi wa kwanza wa mwaka huu.

Katika mchezo wa mapema leo Aston Villa wanaingia wakiwa na morali ya juu baada ya ushindi wa mabao 4-3 dhidi ya Sunderland, ambapo Kocha Unai Emery akiwa na rekodi ya ushindi dhidi ya Fulham, huku mshambuliaji Ollie Watkins akiwa na rekodi nzuri ya kufunga dhidi ya timu hiyo.

EP 03

Liverpool wanatarajiwa kushinda dhidi ya Crystal Palace licha ya kuwa na rekodi isiyoridhisha katika mechi za nyumbani dhidi yao hivi karibuni, huku West Ham United na Everton wakitarajiwa kuwa na mechi isiyotabirika ambapo hakuna timu inayoonekana kuwa na ubora kuliko nyingine.

Kwa upande mwingine, Tottenham watakutana na Wolves katika mechi ambayo inaonekana kuwa ngumu kutabiri, licha ya Wolves tayari imeshashuka daraja. Spurs wanahitaji ushindi ili kujiokoa. Katika mchezo wa kuvutia zaidi leo, Jumamosi, Arsenal wanapewa nafasi kubwa ya kushinda dhidi ya Newcastle, huku presha ikizidi kuongezeka kwa kocha Eddie Howe kufuatia matokeo mabaya ya hivi karibuni. Newcastle haijashinda katika michezo 13 ya mwisho ugenini dhidi ya Arsenal.

Kwa ujumla, raundi ya 34 inaonekana kuwa na ushindani mkubwa na inaweza kuwa na athari kubwa katika mbio za ubingwa, nafasi za kufuzu mashindano ya Ulaya na vita ya kushuka daraja, huku supercomputer ya Opta ikitoa mwanga wa kile kinachoweza kutokea, lakini matokeo halisi yataamuliwa uwanjani.