Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ubelgiji: Hatuogopi uenyeji wa Marekani

UBELGIJI Pict

Muktasari:

  • Kuelekea mechi hiyo, Marekani inaonekana nje ya uwanja kuwa tishio kutokana na kuwepo matarajio ya umati mkubwa wenye msisimko na mashabiki wao huko Seattle, lakini Ubelgiji wanasema hawaogopi mazingira yatakayowakabili.

WASHINGTON, MAREKANI: ALFAJIRI ya kuamkia Jumanne kwa saa za Afrika Mashariki, wenyeji wenza wa Kombe la Dunia 2026, Marekani wataikaribisha Ubelgiji kwenye mechi ya hatua ya 16 bora kuwania kufuzu robo fainali.

Kuelekea mechi hiyo, Marekani inaonekana nje ya uwanja kuwa tishio kutokana na kuwepo matarajio ya umati mkubwa wenye msisimko na mashabiki wao huko Seattle, lakini Ubelgiji wanasema hawaogopi mazingira yatakayowakabili.

“Nafikiri tunachotakiwa kufanya ni kuonyesha ujasiri uwanjani,” amesema beki wa kushoto wa Ubelgiji, Maxim De Cuyper.

“Jaribu kucheza mchezo wako mwenyewe. Ukicheza dhidi ya mashabiki 80,000 au ukiwa nao 80,000, lazima ujaribu kufanya kitu kilekile.”

Marekani wamekuwa wakifurahia sapoti kubwa ya mashabiki wa nyumbani katika michuano yote, ikiwemo Seattle, ambapo takribani watu 67,000 walishuhudia Marekani wakiishinda Australia katika mchezo wao wa pili wa makundi.

UBELG 01

“Pindi inapokuwa inakuwa ngumu kidogo kwao, mashabiki wanaweza pia kugeuka dhidi yao, na watakuwa na presha zaidi,” amesema beki Timothy Castagne.

“Kwa hiyo sina tatizo, hainisumbui. Tunacheza na hatusikii kinachoendelea nje ya uwanja.”

Huu hautakuwa mchezo wa kwanza kati ya timu hizi, mara ya mwisho zilikutana Machi 2026 katika mechi ya kirafiki ambapo Ubelgiji ilishinda kwa mabao 5-2 mjini Atlanta, matokeo ambayo yaliibua mashaka makubwa kuhusu nafasi ya Marekani kwenye michuano hii.

“Wamekuwa wakiboresha sana tangu mchezo wa kirafiki uliopita,” amesema Dodi Lukebakio, ambaye alifunga mabao mawili katika ushindi huo wa 5-2.

De Cuyper alionya dhidi ya kutoa hitimisho kubwa kutokana na ushindi wa Ubelgiji mwezi Machi, akisema matokeo hayo yalitoa picha isiyo sahihi sana. Pia alimpongeza Senne Lammens kwa uchezaji wake katika mchezo huo, akisema matokeo yangeweza kuwa tofauti bila mchango wa kipa huyo.

UBELG 02

“Ilikuwa tayari inasemwa wakati huo kwamba huenda tukakutana na Marekani kwenye Kombe la Dunia,” amesema De Cuyper.

“Bila shaka, wachezaji wengi hawakuwepo wakati huo. Lakini ni faida kwamba tayari tumeiona. Tunachukua mambo kutoka hapo. Ingawa bado inabaki kuonekana watakuja vipi.”

Marekani watamkosa mshambuliaji Folarin Balogun, ambaye amesimamishwa baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu dhidi ya Bosnia and Herzegovina.

Balogun amekuwa miongoni mwa wachezaji hatari zaidi wa Marekani kwenye Kombe la Dunia, lakini De Cuyper alikwepa kutoa maelezo kuhusu jinsi timu yao itakavyokabiliana na mabadiliko ya washambuliaji.

“Sipendi kusema sana kuhusu ni sifa zipi ni bora,” amesema.

“Wana hatari nyingi kwenye timu.”

Kiungo mkongwe wa Ubelgiji, Axel Witsel amesema: “Italazimika kuendana na ukweli kwamba wanacheza na mabeki watatu nyuma. Nafikiri tuna silaha za kuwadhuru. Tayari tulifanya hivyo kwenye mchezo wa kirafiki Machi, lakini leo mazingira ni tofauti kabisa katika uwanja utakaokuwa wa kwao pekee dhidi yetu.”