Tuchel aweka rekodi, akiibamiza Atletico

MADRID, HISPANIA. NI utamu huko Ligi ya Mabingwa barani Ulaya ambapo mashabiki wa Chelsea wana furaha zaidi baada ya timu yao kuibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya mtoano ya 16, ikiwa ugenini dhidi ya Atletico Madrid.
Chelsea ilijipatia bao katika dakika ya 68 kupitia straika wake Olivier Giroud aliyepiga Tik taka mpira uliokuwa umepigwa na mabeki wa Atletico na kuzagaa kwenye eneo la boksi.
Baada ya Chelsea kushinda mchezo huo Thomas Tuchel aliweka rekodi yakuwa kocha wa tatu katika historia ya timu hiyo kuwahi kushinda mchezo wa kwanza wa UEFA akiwa ameikuta timu kwenye hatua ya mtoano, makocha wengine waliowahi kufanya hivi ni Roberto Di Matteo and Guus Hiddink. Baptism.
Tuchel pia aliweka rekodi yakuwa kocha wa pili kuiongoza Chelsea katika mechi nane na kuruhusu mabao machache, akiruhusu mawili. Kocha anayeshikilia nafasi ya kwanza ni bwatukaji Jose Mourinho  aliyeiongoza kwenye mechi nane na ikaruhusu bao moja.


Mchezo mwingine uliopigwa hapo jana ulikua kati ya Lazio iliyokua nyumbani dhidi ya Bayern Munich na Munich ikashinda mabao 4-1.