Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tottenham Hotspur yamnasa Mateus Fernandes

SPURS Pict

Muktasari:

  • Spurs haijaweka wazi muda wa mkataba wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21, ambaye ameichezea timu ya taifa ya Ureno mara moja lakini hakujumuishwa katika kikosi cha Kombe la Dunia.

LONDON, ENGLAND: TOTTENHAM Hotspur imekamilisha usajili wa kiungo Mateus Fernandes kutoka West Ham kwa ada iliyovunja rekodi ya klabu hiyo ya pauni85 milioni.

Spurs haijaweka wazi muda wa mkataba wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21, ambaye ameichezea timu ya taifa ya Ureno mara moja lakini hakujumuishwa katika kikosi cha Kombe la Dunia.

Fernandes ametumia misimu miwili iliyopita katika Ligi Kuu ya England akiwa na Southampton na West Ham, ingawa klabu zote mbili zilishuka daraja kwenda Championship katika vipindi tofauti.

"Nimemfuatilia Mateus kwa muda mrefu kwa sababu anaunganisha ubora akiwa na mpira pamoja na nguvu, akili na kasi ya mchezo ambayo ni muhimu sana katika mfumo tunaotaka kucheza," amesema kocha mkuu wa Spurs, Roberto De Zerbi.

"Licha ya umri wake mdogo, tayari ana uzoefu mzuri wa Ligi Kuu ya England na ameonyesha kiwango bora pamoja na uthabiti katika kiwango hiki."

SPU 01

"Anajiamini akiwa hana presha, ana uwezo wa kuusogeza mpira mbele, anafanya kazi kwa bidii kwa ajili ya timu na ana ujasiri wa kubadilisha mchezo katika nyakati ngumu."

"Ninaamini hii ndiyo mazingira sahihi kwake kuendelea kuimarika."

Tottenham iliwashinda wapinzani kadhaa waliokuwa wanamwania, akiwemo Manchester United, ambao hawakuwa tayari kufikia kiwango cha fedha kilichokubaliwa na Spurs pauni 85milioni zinazolipwa moja kwa moja bila nyongeza yoyote ya bonasi.

Fernandes alikuwa mmoja wa malengo makuu ya klabu hiyo ya London Kaskazini baada ya Newcastle kukataa ofa ya Spurs kwa ajili ya kiungo wa Italia, Sandro Tonali.

SPU 02

Hata hivyo, Spurs sasa imekubaliana na Newcastle kuhusu ada ya pauni100 milioni kwa ajili ya Tonali, jambo linaloweza kufanya usajili huo kukamilika hivi karibuni.


Tottenham imeanza kwa kasi dirisha la usajili wa majira ya joto, huku Fernandes akiwa usajili wao wa tano tayari.

Amefuata nyayo za kipa Martin Dubravka pamoja na mabeki Marcos Senesi, Andy Robertson na Jan Paul van Hecke ambao tayari wamewasili klabuni hapo.

"Ninafuraha kwa hatua hii mpya katika maisha yangu ya soka," amesema Fernandes.

"Spurs ni klabu kubwa na kocha mkuu alikuwa sababu muhimu iliyonifanya nichague kujiunga hapa."

"Tulipozungumza, ilikuwa ni mazungumzo maalumu sana. Tuna mtazamo unaofanana kuhusu soka, kuingia uwanjani kama timu imara, yenye mapambano na nguvu, na kupigania ushindi katika kila mechi."