Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Timu tano Mabingwa Ulaya bado England

MABINGWA Pict

Muktasari:

  • Newcastle ilinufaika na kushika nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi Kuu England msimu uliopita na kufanikiwa kukamatia tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya.

LONDON, ENGLAND: ENGLAND inaendelea kushikilia tiketi ya kuwa na timu tano kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao kutokana na kufanya vizuri kwenye michuano ya Ulaya kwa wiki iliyopita.

Timu nane kati ya tisa za Ligi Kuu England zilishinda, huku Chelsea ikibaki kuwa yenyewe tu iliyochapwa.

Arsenal iliendelea na rekodi yake ya ushindi wa asilimia 100 kwa ushindi kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya na hivyo kushika usukani kwenye msimamo wa timu 36, huku Manchester City ikishika namba nne na Liverpool, Spurs, Newcastle na Chelsea zote zikifanikiwa kuwamo kwenye 13 bora.

Aston Villa ushindi wake huko Basel uliwafanya kushika namba tatu kwenye msimamo wa Europa League, wakati Nottingham Forest ilipanda hadi nafasi ya 11 baada ya ushindi wake dhidi ya Utrecht.

Na Crystal Palace, ambayo inachuana kwenye Conference League ilipanda hadi kwenye nafasi ya tisa baada ya ushindi dhidi ya Shelbourne. Kutokana na kupata uhakika wa bonasi ya pointi zinazotokana na timu za Arsenal, Man City na Aston Villa zitaifanya England kuwa na uhakika wa kuendelea kuwa na timu tano kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Kwenye mchakato wa chati za Uefa ni kwamba England sasa pointi zake zimeongezeka na kufikia 13.166 na hivyo kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kuwa na tiketi ya ziada kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Pointi hizo zinawafanya kuwa juu kwa tofauti ya pointi mbili juu ya nchi inayoshika nafasi ya tatu, Italia yenye pointi 11.071. Na hata nchi inayoshika nafasi ya pili, Ujerumani iliyozidiwa pointi za moja na nusu na England, ikiwa na 11.66.

Kwa hesabu za msimu huu, timu za Ligi Kuu England zimeshinda mechi 34 kati ya 51 na kuchapwa mara 12 tu.

Kwa kulinganisha na Bundesliga, Serie A na LaLiga timu za ligi hiyo, kila moja imeshinda mechi 22.

Newcastle ilinufaika na kushika nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi Kuu England msimu uliopita na kufanikiwa kukamatia tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya.