Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tiketi ya Man United Vs Spurs ni mshahara mpya wa Fei Toto

TIKETI Pict

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa Daily Mail, kampuni ya Vivid Seats ambayo tajiri, Boehly anahusika nayo inauza tiketi za “prime seats” (viti vya hadhi ya juu) kwenye mstari wa kati kwa Pauni 22,738 kwa mechi ya Manchester United dhidi ya Tottenham itakayofanyika San Mames, Bilbao, Mei 21.

LONDON, ENGLAND: MACHESTER United na Tottenham Spurs wanasubiri kitu kimoja tu msimu huu kiwape japo furaha.

Fainali ya Europa. Itapigwa Jumatano ijayo, lakini kuna kitu amefanya mmiliki mwenza wa klabu ya Chelsea kikawakera mashabiki wa soka Ulaya huku Wabongo wakikumbuka mshahara mpya wa Feitoto anayekipiga Azam Fc.

Tovuti inayomilikiwa na mmiliki mwenza wa Chelsea, Todd Boehly, inauza tiketi za fainali ya Europa League kwa takribani Pauni 23,000 (Sh82 milioni).

Mwanaspoti linajua huo ni sawa na mshahara mpya ambao Azam FC, imemuahidi staa wake Feitoto ili asaini mkataba mpya wa kuitumikia klabu hiyo kuanzia msimu 2026/27. 

Hatahivyo, Feitoto inaelezwa ameidengulia Azam na imeamua kusitisha mazungumzo nae kuhusu mkataba kwani inadaiwa kila ikimuita mezani kwa mazungumzo anakwenda na madai mapya tofauti na ya makubaliano ya kikao kilichopita. Simba na Yanga zinatajwa kumshawishi Feitoto ajiunge nao pindi mkataba utakapomalizika.

Ulaya sasa. Kwa mujibu wa Daily Mail, kampuni ya Vivid Seats ambayo tajiri, Boehly anahusika nayo inauza tiketi za viti vya hadhi ya juu(Prime Sites) kwenye mstari wa kati kwa Pauni 22,738 kwa mechi ya ManUnited dhidi ya Tottenham itakayopigwa San Mames, Bilbao, Mei 21.

Kwa mujibu wa shirika la IQ, Boehly anamiliki asilimia 41 ya tovuti hiyo ya tiketi kupitia kampuni yake, Eldridge Industries. Mbali ya tiketi hizo, pia kuna nyingine zinazouzwa kati ya Pauni 55 hadi 204, pamoja na nyingine zenye bei ya juu zaidi.

Mashabiki wamekosoa vikali suala hili kwani bei za awali za tiketi hizi ilikuwa ni Pauni 1800 pekee lakini imepanda mara dufu hali inayowanyima wengi kwenda kutazama mchezo huo.

Machi mwaka huu kikundi cha Chelsea Supporters Trust (CST) kililalamikia uhusiano huu kati ya Boehly na tovuti hiyo ya tiketi wakitaka kwenda bodi ya Ligi Kuu ili hatua zichukuliwe.

Barua yao ilisomeka: “Kama Mkurugenzi wa Chelsea FC na mmiliki wa timu, Boehly uhusiano wake na Vivid Seats ni usiofaa kabisa na unadhoofisha kwa kiasi kikubwa juhudi za Chelsea FC, ligi kuu na Polisi wa Jiji la London katika kupambana na uuzaji haramu wa tiketi.”

Hata hivyo, tangu kutolewa kwa malalamiko hayo, sio Boehly wala wawakilishi wake waliojibu na tiketi bado zinaendelea kuuzwa kwenye tovuti ya Vivid Seats.”