Ten Hag amvisha mabomu Rashford

MANCHESTER, ENGLAND. KOCHA wa Manchester United Erik Ten Hag amemvisha mabomu straika wake Murcus Rashford kwa kumpa jukumu la kuongoza eneo la ushambuliaji kwenye mechi ya leo dhidi ya Manchester City inayotarajiwa kupigwa leo, Jumapili katika Dimba la Etihad.
Rashford atakuwa na kazi ngumu ya kuhakikisha anafunga mabao ya kutosha na kuiwezesha Man United kushinda mbele ya Man City ambayo safu yao ya ushambuliaji inaongozwa na Erling Haaland aliye kwenye kiwango bora tangu ajiunge nao.
Man United inatarajiwa kuendeleza moto wake kwenye EPL ambapo hadi sasa imeshinda mechi nne mfululizo ikiwa pamoja na il ya Arsenal.
Rashford naye amekuwa kwenye kiwango bora na mchezo wa mwisho dhidi ya Arsenal alifunga mabao mawili na kutoa asisti moja.
Haaland kwa upande wa Man City yeye amefunga mabao 11 katika mechi saba na mechi zoteĀ  za ligi alizocheza amefunga.
Kikosi cha Man United, David de Gea, Diogo Dalot, Malacia, Martinez, Raphael Varane, Scott Mctominay, Christian Eriksen, Marcas Rashford, Bruno Fernandes, Antony na Jadon Sancho.
Man City, Ederson, Kayle Walker, Joao Cancelo, Nathan Ake, Manuel Akanji, Gundogan, Benardo Silva, Kevin de Bruyne, Erling Haaland, Jack Grealish, Phil Foden.