Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TEAM MONEY: Kikosi cha Kwanza cha wanaolipwa mshahara mkubwa 2025-26

MONEY Pict

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa mtandao wa Capology unaotoa taarifa za mishahara ya wanasoka Ulaya, umeweka hadharani kikosi cha kwanza kinachoundwa na mchezaji anayelipwa mkwanja mrefu kwenye kila namba. Kikosi hicho kinatumia fomesheni ya 4-4-2.

LONDON, ENGLAND: MIAMBA ya soka ya Hispania, Real Madrid inatawala soka la Ulaya kwenye kikosi cha kwanza cha mastaa wanaolipwa mishahara mikubwa zaidi msimu huu wa 2025-26, lakini timu hiyo ina majina ya masupastaa wa maana kutoka Bayern Munich, Liverpool, PSG, Manchester United na Manchester City.

Kwa mujibu wa mtandao wa Capology unaotoa taarifa za mishahara ya wanasoka Ulaya, umeweka hadharani kikosi cha kwanza kinachoundwa na mchezaji anayelipwa mkwanja mrefu kwenye kila namba. Kikosi hicho kinatumia fomesheni ya 4-4-2.


Kipa: Manuel Neuer – Euro 403,846 kwa wiki

Kipa namba moja wa Bayern Munich, Manuel Neuer amepata nafasi mbele ya Mjerumani mwenzake Marc-Andre ter Stegen ambaye analipwa Euro 320,577 kwa wiki huko Barcelona. Kwa maana hiyo Neuer ndiye kipa anayelipwa mshahara mkubwa zaidi huko Ulaya kwa sasa.


Beki wa kulia: Trent Alexander-Arnold – Euro 320,577 kwa wiki

Nahodha wa Chelsea, Reece James alikuwa beki wa kulia wa kikosi hicho kwa msimu uliopita, lakini sasa amepoteza namba mbele ya Mwingereza mwenzake baada ya kujiunga na Real Madrid. Trent analipwa Euro 320,577 huko Bernabeu alikojiunga kwenye dirisha hili la kiangazi.

MONE 01

Beki wa kati: Virgil Van Dijk – Euro 405,948 kwa wiki

Bado anaendelea kuhesabika kama mmoja wa mabeki wa kati bora kabisa duniani. Hilo linakwenda sambamba na mshahara anaolipwa mkali huyo huko kwenye kikosi cha Liverpool anakocheza, ambako kwa wiki anaweka mfukoni, Euro 405,948.


Beki wa kati: David Alaba – Euro 432,692 kwa wiki

Real Madrid ilikwenda kunasa saini ya beki David Alaba mwaka 2021 kutoka Bayern Munich na kumsainisha dili linalomwingizia mshahara mnono. Hata hivyo, Alaba amekuwa na bahati mbaya tangu alipotua Bernabeu, ambapo majeraha ya goti yamemuaka nje kwa muda mrefu.


Beki wa kushoto: Lucas Hernandez – Euro 253,846 kwa wiki

Anacheza kwenye kikosi cha Paris Saint-Germain kilichowahi kuwa na mastaa wa maana kama Sergio Ramos, Lionel Messi, Neymar na Kylian Mbappe, lakini beki huyo wa kushoto anabaki kuwa mchezaji pekee wa kikosi cha kocha Luis Enrique kilichobeba mataji matatu msimu uliopita kuingia kwenye kikosi hiki.

MONE 02

Winga wa kulia: Mohamed Salah – Euro 463,940 kwa wiki

Staa mwingine aliyekuwa akiibua maswali mengi juu ya mkataba wake kwenye kikosi cha mabingwa Liverpool, ambaye alikubali kubaki kwa kusaini dili jipya, ambalo linamfanya aendelee kubaki kwenye orodha ya wachezaji wanaolipwa mshahara mkubwa kwa mawinga wa kulia.


Kiungo wa kati: Casemiro – Euro 405,948 kwa wiki

Kiungo huyo wa Kibrazili alianza maisha yake vizuri sana huko Manchester United kabla ya mambo kugeuka na kucheza kwa kiwango cha hovyo sana msimu uliopita. Lakini, Casemiro ndiye mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa Man United na kwenye nafasi yake anayocheza ya kiungo wa kati.


Kiungo wa kati: Jude Bellingham – Euro 400,577 kwa wiki

Si tu Real Madrid ilitoa Euro 103 milioni kunasa huduma ya kiungo Jude Bellingham kutoka Borussia Dortmund, lakini ilimfanya pia kuwa mmoja wa viungo wanaolipwa mshahara mkubwa, ambapo staa huyo anakadiliwa kupokea Euro 21 milioni kwa mwaka.

MONE 03

Winga wa kushoto: Vinicius Junior – Euro 400,577 kwa wiki

Mambo yanakuwa moto kwelikweli linapokuja suala la mazungumzo ya mkataba wa staa huyo wa Kibrazili. Klabu kadhaa za Saudi Arabia zinahitaji saini yake, lakini Real Madrid imemtuliza kwenye kikosi chake kwa kumlipa mshahara mkubwa, Euro 400,577 kwa wiki.


Mshambuliaji: Erling Haaland – Euro 608,922 kwa wiki

Straika, Erling Haaland ndiye mwanasoka anayelipwa mshahara mkubwa kuliko wote kwenye soka la Ulaya kwa sasa, ambapo klabu yake ya Manchester City inamlipa Euro 31 milioni kwa mwaka huku mkataba wake ukitarajia kufika kikomo 2034.

MONE 04

Mshambuliaji: Kylian Mbappe – Euro 600,962 kwa wiki

Haaland na Mbappe wamekuwa kwenye maelezo ya kizazi kipya kwamba ni majibu ya mastaa Messi na Ronaldo. Wawili hao bado hawajashinda Ballon d’Or, huku Mbappe akisubiri pia taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya. Huduma yake huko Real Madrid inamshuhudia akilipwa mshahara mkubwa.