Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha Scotland akimbia mahojiano

Muktasari:

  • Kipigo hicho kilichotokea jijini Miami, Florida, kimeiacha Scotland katika hali ngumu ya kusubiri matokeo ya makundi mengine ili kujua kama itafanikiwa kutinga hatua ya 32 bora kupitia nafasi za timu bora zilizomaliza katika nafasi ya tatu.

FLORIDA, MAREKANI: KOCHA wa Scotland, Steve Clarke, ameshindwa kuficha hasira zake baada ya timu yake kuchapwa mabao 3-0 na Brazil katika mchezo wa mwisho wa Kundi C wa Kombe la Dunia 2026, kiasi cha kuondoka katikati ya mahojiano ya moja kwa moja ya televisheni mara tu baada ya mechi kumalizika.

Kipigo hicho kilichotokea jijini Miami, Florida, kimeiacha Scotland katika hali ngumu ya kusubiri matokeo ya makundi mengine ili kujua kama itafanikiwa kutinga hatua ya 32 bora kupitia nafasi za timu bora zilizomaliza katika nafasi ya tatu.

Matarajio ya Scotland yalikuwa makubwa baada ya kuanza mashindano kwa ushindi dhidi ya Haiti, lakini baadaye ilipoteza mechi mbili mfululizo dhidi ya Morocco na Brazil na kujikuta ikimaliza kundi ikiwa na pointi tatu pekee.

Katika mahojiano yake na BBC baada ya mchezo huo, Clarke alionekana mwenye huzuni na hasira kutokana na namna timu yake ilivyopoteza mchezo muhimu.

Alipoulizwa kuhusu ugumu wa mchezo huo dhidi ya Brazil, kocha huyo mwenye umri wa miaka 62 alijibu kwa kifupi: "Tulijifanyia ugumu wenyewe, hivyo ndivyo ilivyokuwa."

Alipoendelea kuulizwa kama makosa ya wachezaji wake ndiyo yaliyoipa Brazil nafasi ya kushinda kwa urahisi, Clarke hakuficha masikitiko yake.

"Tuliwapa mabao, tuliwapa mchezo waliokuwa wanauhitaji. Inasikitisha."

Hata hivyo, wakati mwandishi alipomuuliza kuhusu uwezekano wa Scotland kufuzu na hesabu za timu bora zitakazomaliza nafasi ya tatu, Clarke alionekana kuchoshwa kabisa na mjadala huo.

Badala ya kujibu, alikatisha mahojiano ghafla na kuondoka mbele ya kamera huku akiinua mkono kuashiria kuwa hataki kuendelea kuzungumza.