Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Straika mpya Arsenal bado kizunguzungu

GYOKERES Pict

Muktasari:

  • Lakini, wakati ikifahamu wazi kwamba inapaswa kuchagua mmoja kwenye orodha ya mastraika hao wawili, mkurugenzi wa michezo wa miamba hiyo ya Emirates, Andrea Berta, ameweka milango wazi ya kuzungumza na wachezaji wote hao wawili ili kumnasa mmoja.

LONDON, ENGLAND: ARSENAL sasa imebaki na uamuzi kwenye mikono yake wenyewe juu ya mastraika inayowasaka kwenye dirisha hili, ambapo kwenye meza yao kuna majina ya wakali wawili, Viktor Gyokeres na Benjamin Sesko.

Lakini, wakati ikifahamu wazi kwamba inapaswa kuchagua mmoja kwenye orodha ya mastraika hao wawili, mkurugenzi wa michezo wa miamba hiyo ya Emirates, Andrea Berta, ameweka milango wazi ya kuzungumza na wachezaji wote hao wawili ili kumnasa mmoja.

Lakini, wakati ukipasua kichwa juu ya nani atatua Emirates kati ya Gyokeres na Sesko, bosi huyo amefungua milango pia ya kumsaka straika wa Aston Villa, Ollie Watkins, ambaye yupo kwenye rada za timu hiyo tangu kwenye dirisha la Januari iliposhindwa kidogo kuinasa saini yake.

Huko nyuma, Arsenal ilikuwa ikisaka pia huduma ya mastraika Alexander Isak wa Newcastle United na Julian Alvarez wa Atletico Madrid, lakini Gyokeres na Sesko ndio hao ambao wanapewa nafasi kubwa ya kunaswa.

Ripoti zinafichua kwamba straika Gyokeres amechagua kwenda Arsenal mbele ya timu nyingine zinazomhitaji ikiwamo Manchester United na timu za Hispania na Italia.

Gyokeres, 27, ameitaka timu yake kumruhusu kuondoka kwa ada inayoanzia Pauni 60 milioni. Lakini, rais wa Sporting, Frederico Varandas alisema hayupo tayari kumwaachia straika huyo aondoke kwa pesa ndogo.

Sesko, 22, naye anaweza kuruhusiwa na timu yake ya RB Leipzig kwa ada ya Pauni 60 milioni na staa huyo wa Slovenia alikaribia kujiunga na Arsenal kwenye dirisha la majira ya kiangazi la mwaka jana.

Hata hivyo, kuna klabu nyingine zinamtaka Sesko ikiwamo Bayern Munich jambo linalofanya vita ya kufukuzia saini yake kuwa kali na Arsenal kufikiria saini nyingine, ikiwamo ya Watkins.

Arsenal inahitaji kuboresha safu yake ya ushambuliaji baada ya msimu uliopita washambuliaji Kai Havertz na Gabriel Jesus kushindwa kuonyesha makali ya maana kabla ya kupata majeruhi na kuigharimu timu.

Kutokana na hali ilivyo, Arsenal inaonekana bado haijafanya uamuzi wa mwisho wa kuhusu straika gani inamtaka baina ya Gyokeres, Sesko na sasa watkins, wakati dirisha refu la majira haya ya kiangazi likifunguliwa tayari Jumatatu hii Juni 16, 2025.