Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Steven Gerrard afichua waliomvuruga akiwa dimbani

GERRARD ST Pict

Muktasari:

  • Watatu hao wametajwa na gwiji wa Liverpool, Steven Gerrard alipokuwa akizungumza kupitia YouTube chanel ya "Rio Ferdinand Presents", baada ya kutakiwa kuwataja wachezaji ambao waliwahi kumpa changamoto akiwa kwenye majukumu yake uwanjani.

Waliokuwa viungo wa Barcelona Xavi Hernandez, Andres Iniesta na Sergio Busquets wametajwa kama wapinzani wa kweli walipokuwa katika majukumu ya kuitumikia klabu hiyo ya Hispania, hasa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Watatu hao wametajwa na gwiji wa Liverpool, Steven Gerrard alipokuwa akizungumza kupitia YouTube chanel ya "Rio Ferdinand Presents", baada ya kutakiwa kuwataja wachezaji ambao waliwahi kumpa changamoto akiwa kwenye majukumu yake uwanjani.

Gerrard amesema aliwahi kukutana na Xavi, Iniesta, na Busquets kwa nyakati tofati, na wote walionyesha kuwa kwenye kiwango bora zaidi, hali ambayo ilimpa wakati mgumu yeye kama kiungo na wachezaji wengine wa Liverpool.

GERRA 03

Amesema amekutana na wachezaji wengi wanaocheza nafasi kiungo, lakini kila anapojifanyia tathini hawa jamaa watatu, wanaendelea kumthibitishia walikuwa tishio na walijua nini wanakifanya uwanjani.

"Kuna baadhi ya viungo ambao sikupendezwa kucheza nao. Hasa wale wa aina ya Barcelona. Walipokuwa pamoja kwa wakati mmoja, kwa mtu wa aina yangu ambaye anapenda kucheza kwa nguvu na kuacha alama, walikuwa wagumu sana kuwashinda.

"Xavi, Busquets na Iniesta, huo ulikuwa mchanganyiko mkali sana wa kiungo. Nikimtazama Pedri sasa na wachezaji wa aina hiyo, hao ndio walikuwa changamoto kubwa zaidi kwangu.

GERRA 02

“Hawa jamaa sitawasahau kabisa, walicheza kwa ushirikiano wakati wote, walitimiza lengo la kile walichotakiwa kukifanya katika safu ya kiungo, lakini pamoja na yote hayo, nilipokutana nao kwa kushirikiana na wachezaji wengine wa Liverpool, tulijitahidi kupambana nao, na wakati mwingine tulifanikiwa kuwashinda.” amesema.

Gerrard, ambaye anatambuliwa kama mmoja wa viungo bora zaidi wa kizazi chake, pia amekiri kwamba huenda asingepata heshima sawa kama angecheza katika kizazi cha sasa kutokana na jinsi mchezo wa soka kubadilika kwa kiasi kikubwa.

"Sina uhakika kama ningeweza kuheshimiwa kama nilivyoheshimiwa wakati wa kazi yangu kama ningekuwa nacheza katika kipindi hiki.

"Nafikiri soka limebadilika sana, mchezo huu umekuwa wa kimkakati sana. Kanuni zimebadilika na kuendelea. Uchezaji wa nguvu, kuacha alama, sasa soka ni laini zaidi, rafiki zaidi kwa wachezaji na salama zaidi.

GERRA 04

"Napenda soka la kizazi kilichopita, hilo ndilo nililocheza. Lakini sasa mchezo unahusisha hadi teknolojia, unaweza kupewa kadi na kutolewa nje kwa kosa dogo sana.

"Hilo ndilo linalonitia wasiwasi: Je, ningekuwa Steven Gerrard yule wa zamani katika kizazi cha sasa? Sijui. Ingebidi nijibadilishe na hilo lingeondoa mengi kwenye mtindo wangu wa uchezaji," amesema.