Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sterling mbaroni

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

  • Polisi walimsimamisha mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 kwenye barabara ya M3 huko Hampshire, saa 3 asubuhi, juzi na baada ya muda Sterling ambaye kwa sasa anachezea Feyenoord ya Uholanzi aliachiwa kwa dhamana huku uchunguzi ukiendelea.

LONDON, ENGLAND: NYOTA wa zamani wa soka wa England, Raheem Sterling, amekamatwa kwa tuhuma za kuendesha gari akituhumiwa kuwa alikuwa ametumia dawa zinazodaiwa kuwa za kulevya baada ya kusababisha ajali kwa kugonga kizuizi cha barabarani.

Polisi walimsimamisha mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 kwenye barabara ya M3 huko Hampshire, saa 3 asubuhi, juzi na baada ya muda Sterling ambaye kwa sasa anachezea Feyenoord ya Uholanzi aliachiwa kwa dhamana huku uchunguzi ukiendelea.

Wakati anakamatwa mchezaji huyo alidaiwa kuendesha gari akiwa ametumia dawa za kulevya jambo lililochangia akagonga kizuizi na kuharibu sehemu ya gari lake aina ya Lamborghini. Sterling aliyezichezea Liverpool, Chelsea na Manchester City alikuwa akisafiri kwa spidi kubwa jambo lililowashtua polisi wa usalama barabarani na walipokuwa akimfuatilia kwa nyuma aliparamia kizuizi akilenga kuwakimbia.

Sterling, ambaye aliachwa na Chelsea, Januari, kabla ya kusaini Feyenoord ya Uholanzi, amekuwa akipitia kipindi kigumu, kwa mujibu wa watu wake wa karibu. Miongoni mwa mashtaka aliyofunguliwa ni pamoja na matumizi ya dawa za kulevya, kuendesha gari kwa spidi isiyotakiwa, kumiliki dawa hizo na kugoma kutoa sampuli ya damu kwa ajili ya vipimo.

Kwa mujibu polisi, dawa alizokutwa nazo zinajumuisha za usingizi, maumivu pamoja na steroidi, gesi ya 'kuchekesha' na GHB.

Polisi wa Hampshire walisema: “Hakuna gari lingine lililohusika na hakuna majeruhi walioripotiwa. Dereva, mwanaume mwenye umri wa miaka 31 kutoka Berkshire, amekamatwa kwa tuhuma za kuendesha gari akiwa hana uwezo kutokana na matumizi ya dawa za kulevya, kuendesha kwa hatari, kumiliki dawa za kundi C na kushindwa kutoa sampuli ya damu. Ameachiwa kwa dhamana huku uchunguzi wetu ukiendelea.”

Sterling alikuwa na umri wa miaka 15 tu aliponunuliwa na Liverpool kutoka akademi ya QPR 2010, ambako alikuwa kipenzi cha mashabiki wa Anfield kabla ya mgogoro wa mkataba kumfanya ahamie Manchester City 2015. Akiwa huko alipata mafanikio makubwa akishinda mataji manne ya Ligi Kuu England, Carabao mara tano na FA mara moja.

Baadaye alipitia vipindi visivyo na mafanikio makubwa akiwa Chelsea na Arsenal, kabla ya kuhamia Feyenoord kama mchezaji huru mwaka huu.

Sterling pia ameichezea England mara 82 na kufunga mabao 20. Chanzo cha karibu na nyta huyo kilisema: “Alikuwa mchezaji mahiri wa kimataifa wa England ambaye ameisaidia kufikia mafanikio makubwa katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, lakini katika miaka ya karibuni amefanywa ajisikie hana thamani na amesahaulika. Mzigo wa kisaikolojia alionao hauwezi kupimika.”