Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha Afrika Kusini ajiweka njia panda

BROOS Pict

Muktasari:

  • Kauli hiyo inakuja huku kukiwa na matamanio makubwa kutoka kwa mashabiki na wadau wa soka wanaotaka kuona mwelekeo wa kikosi hicho baada ya kuishia hatua ya mtoano kwenye Kombe la Dunia kwa kufungwa na Canada bao 1-0. 

Kocha wa Afrika Kusini, Hugo Broos, amebadili kauli yake akisema kwamba, atajipa muda wa kutafakari kabla ya kufanya uamuzi wa mwisho wa kuachana na timu hiyo, huku akisema milango bado iko wazi kuendelea kuinoa timu hiyo. 

Kauli hiyo inakuja huku kukiwa na matamanio makubwa kutoka kwa mashabiki na wadau wa soka wanaotaka kuona mwelekeo wa kikosi hicho baada ya kuishia hatua ya mtoano kwenye Kombe la Dunia kwa kufungwa na Canada bao 1-0. 

Broos amesisitiza umuhimu wa kufanya uamuzi kwa utulivu bila kukurupuka, ili kuhakikisha hatua inayofuata inaleta tija kwake na Chama cha Soka Afrika Kusini (SAFA).

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 74, kabla ya hapo amewahi kusema baada ya Fainali za Kombe la Dunia 2026, atastaafu kufundisha soka, hali iliyofanya SAFA kuanza mchakato wa kumsaka mrithi wake huku majina kadhaa ya makocha yakitajwa akiwemo Pitso Mosimane.

Broos akiwa na kikosi cha Afrika Kusini, ameweka rekodi ya kuiongoza timu hiyo kufuzu kwa mara ya kwanza hatua ya mtoano ya Kombe la Dunia, lakini bahati haikuwa yao ikaishia hapo kwa kufungwa na Canada.