Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kisa jela, marafiki wamkimbia Boris Becker

BORIS Pict

Muktasari:

  • Becker, ambaye pia aliwahi kupatikana na hatia ya ukwepaji kodi nchini Ujerumani mwaka 2002, alipelekwa katika gereza la HMP Wandsworth baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili na nusu. Sasa amefunguka jinsi kipindi hicho kilivyobadilisha maisha yake ya kijamii.

ROMA, ITALIA: BINGWA wa zamani wa tenisi  duniani, Boris Becker amesema amepoteza asilimia 95 ya marafiki zake tangu atoke gerezani.

Becker mwenye umri wa miaka 58, ambaye alijizolea umaarufu mwaka 1985 alipokuwa bingwa mwenye umri mdogo zaidi wa mashindano ya Wimbledon Championships kwa upande wa wanaume, alitangazwa kufilisika mwaka 2017 na kufungwa jela mwaka 2022 baada ya kuficha mali na mikopo yenye thamani ya pauni2.5 milioni ili kukwepa kulipa madeni yanayohusiana na kufilisika.

Becker, ambaye pia aliwahi kupatikana na hatia ya ukwepaji kodi nchini Ujerumani mwaka 2002, alipelekwa katika gereza la HMP Wandsworth baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili na nusu. Sasa amefunguka jinsi kipindi hicho kilivyobadilisha maisha yake ya kijamii.

BOR 01

“Unapokuwa gerezani, unapoteza karibu kila kitu. Kinachobaki ni utu na tabia yako. Lazima ujiulize, ‘Mimi ni nani? Hili litanimaliza au litanifanya kuwa imara zaidi?’”

Ameongeza:“Ningesema asilimia 90 ya watu waliokuwa kwenye mzunguko wangu wa karibu wameondoka. Huenda hata ni asilimia 95.”

Mashindano ya Wimbledon yanaanza Jumatatu, lakini Becker bado hawezi kuhudhuria kutokana na masharti ya kuachiliwa kwake mapema. Alitumikia miezi minane gerezani kabla ya kufukuzwa kutoka United Kingdom.

Ingawa yuko kwenye mazungumzo na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Uingereza ili kuondolewa marufuku ya kuingia nchini humo, amesema bado anahisi pengo kubwa kwa kushindwa kurejea Wimbledon.

“Sidhani kama ninaikosa London, lakini ninaikosa Wimbledon. Hapo ndipo maisha yangu ya tenisi yalipoanzia. Nina uhusiano wa karibu sana na klabu hiyo na viwanja vyake. Nina kumbukumbu katika kila uwanja, kila kona, vyumba vya kubadilishia nguo na hata sehemu ya maegesho. Nafikiri ninaijua Wimbledon kuliko mtu mwingine yeyote aliye hai.”

Miaka mitatu na nusu baada ya kuachiliwa kutoka gerezani, Becker anaishi nchini Italia pamoja na mke wake wa tatu, Lillian, na binti yao mdogo Zoe, ambaye ni mtoto wake wa tano.

BOR 02

Ameeleza kuwa hakutaka kuishi tena Ujerumani kwa sababu watu wengi huko walimchukulia kama “mali ya taifa” na hawakuheshimu faragha yake. Anaamini Italia imempa nafasi mpya ya kujenga upya maisha yake.

Becker pia amesema baadhi ya marafiki waliomgeuka wakati wa matatizo yake sasa wanajaribu kurejea katika maisha yake. Hata hivyo, yeye na familia yake wamekuwa waangalifu zaidi baada ya kupitia kipindi kigumu.


Alibainisha kuwa hali hiyo haiwahusu watu wachache waliobaki waaminifu, akiwemo Jurgen Klopp, ambaye aliwahi kujaribu kumtembelea gerezani lakini hakuruhusiwa kwa sababu za kiusalama.

Akihitimisha, Becker amesema:

“Bila shaka kuna watu wanaojaribu kurudi katika maisha yangu. Lakini sasa familia yetu ina mfumo wa kutambua watu wa kuamini. Tukiona ishara za hatari mapema, sina tatizo kuwa mkali na kuwaweka mbali.”