Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Staa Senegal aaga Afcon baada ya kufiwa baba yake

KIUNGO wa Nottingham Forest na timu ya taifa ya Senegal, Cheikhou Kouyate ameondoka kwenye kambi ya Senegal kule nchini Ivory Coast baada ya kufiwa na baba yake.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na chama cha soka cha Senegal, Kouyate alipatwa na msiba wa baba yake Jumanne ya wiki hii na mazishi yanatarajiwa kufanyika leo.

Pia taarifa hiyo inaeleza kwamba Kouyate ameruhusiwa kuondoka kwenye kambi ya Senegal leo kwa ajili ya kwenda Dakar ambako mazishi yatafanyika.

Hakuna uhakika kama staa huyu atarejea kwenye kikosi cha Simba wa Milima ya Teranga baada ya mazishi kwa ajili ya mchezo wa pili wa kundi C dhidi ya Cameroon utakaopigwa Ijumaa Januari 19, saa 2:00 usiku.