Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Liverpool yaikazia Madrid kwa Alexander-Arnold

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Awali Madrid ilidaiwa kuweka pauni 850,000 ili kumpata fundi huyu kabla ya Juni 30 na mkataba wake utakuwa unamalizika kwani wanataka kumtumia kwenye michuano ya klabu bingwa ya Dunia.

INAELEZWA Liverpool wameshikilia msimamo wa kuhitaji Pauni 1 milioni kutoka Real Mªdrid ili kumwachia beki wao wa kimataifa wa England, Trent Alexander-Arnold, 26, kabla ya mkataba wake kumalizika.

Awali Madrid ilidaiwa kuweka pauni 850,000 ili kumpata fundi huyu kabla ya Juni 30 na mkataba wake utakuwa unamalizika kwani wanataka kumtumia kwenye michuano ya klabu bingwa ya Dunia.

Inaelezwa, Liverpool inataka kiasi kikubwa zaidi cha pesa na ikishindikana haitomruhusu staa huyo hadi mkataba wake utakapomalizika.

Moja kati ya sababu za mabosi wa Liverpool kumzuia Trent asiondoke kirahisi kwa sababu haikupendezwa na namna ambavyo taarifa za kuondoka kwa beki huyo kuvuja wakati msimu ukiwa unaendelea na wanaamini baadhi viongozi wa Madrid walihusika kwenye hilo kwani media zilizoripoti kwanza habari hizo zilikuwa ni zile za Hispania.


Florian Wirtz

LIVERPOOL imeingia katika vita dhidi ya Manchester City ili kuipata saini ya mshambuliaji wa Bayer Leverkusen na timu ya taifa ya Ujerumani, Florian Wirtz, 22, katika dirisha lijalo. Hata hivyo, inaonekana kuwa ngumu sana kwa Man City kwa sababu ya kiasi kikubwa cha pesa ambacho kinachotakiwa kuona ni kikubwa sana. Wirtz amekuwa na msimu mzuri na hilo limeziingiza vitani vigogo hao ikiwamo pia Bayern Munich ambayo inapewa nafasi kubwa ya kumbakiza katika Ligi ya Bundesliga.


Marc Guehi

NEWCASTLEcinadaiwa kuwa kwenye nafasi nzuri ya kumsajili beki kisiki wa Crystal Palace na timu ya taifa ya  England, Marc Guehi, 24, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Guehi ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2026, amezivutia timu nyingi kutokana na kiwango alichoonyesha akiwa na Palace na timu  ya taifa ya England kwenye michuano ya Euro mwaka jana. Chelsea pia inatajwa kumwania.


Dean Huijsen

REAL Madrid imeshafikia makubaliao na Bournemouth kwa ajili ya kumsajili beki kisiki wa timu hiyo na Hispania, Dean Huijsen, 22, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi na itatakiwa kulipa Pauni 50 milioni kukamilisha dili hilo. Huijsen ambaye msimu huu amecheza mechi 34 za michuab yote na kufunga mabao manne, mkataba wake wa sasa  unatarajiwa kumalizika mwaka 2030.


Joshua Zirkzee

MSHAMBULIAJI wa Manchester United, Joshua Zirkzee, 23, ni miongoni mwa mastaa walio kwenye rada za Inter Milan inayohitaji kumsajili katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Inaelezwa Inter iko tayari kumsajili fundi huyu licha ya kutoonyesha kiwango bora kwa msimu huu. Zirkzee mwenyewe anatamani sana kuondoka kwa sababu haoni kama yupo kwenye mipango ya kocha wa sasa wa timu hiyo, Ruben Amorim.


Xavi Simons

KIUNGO wa RB Leipzig, Xavi Simons, yuko tayari kuondoka mwisho wa msimu huu licha ya kusaini mkataba wa kudumu Januari mwaka huu. Kiungo huyo wa kimataifa wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 22, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2027, msimu huu amecheza mechi 32 za michuano yote na kufunga mabao 10. Manchester United na Bayern Munich zinatajwa kumwania.


Joan Garcia

BARCELONA wanapanga kushindana na Arsenal katika vita ya kuiwania huduma ya kipa wa Espanyol na timu ya taifa ya Hispania, Joan Garcia, mwenye umri wa miaka 24. Mabosi wa Barcelona wanahitaji sana huduma ya Garcia kwa sababu hawaridhishwi na kiwango cha Wojciech Szczesny ambaye amekuwa langoni baada ya Marc Andre ter Stegen kuumia.


Jonathan Tah

BAYERN Munich imekubali kutoa bonasi ya usajili ya Euro 15 milioni na mshahara wa Euro 12 milioni kwa mwaka ili kumsajili beki wa Bayer Leverkusen na timu ya taifa ya Ujerumani, Jonathan Tah, 29, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Tah ambaye msimu huu amecheza mechi 48 za michuano yote, huduma yake pia inahitajika na Barcelona.