Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Staa Nigeria aliyeumia AFCON, aonekana akicheza Hispania

DAKIKA ya  73 kwenye mchezo wa Copa del Rey nchini Hispania kati  ya Osasuna na Real Sociedad Januari 17, kocha wa Real Sociedad alimnyanyua Umar Sadiq  kutoka benchi na kumuingiza ili achukuwe nafasi ya Andre Silva.

Baada ya kuonekana uwanjani watu wengi walishangazwa na hilo kwani staa huyo wa kimataifa wa Nigeria alikuwa kwenye kikosi cha timu hiyo ya taifa kule Abidjan akijiandaa kwa ajili ya kucheza kwenye fainali za AFCON 2023.

Lakini wakati mashindano yamebakiza siku mbili kabla ya kuanza staa huyo alidaiwa kupatwa na majeraha ya goti ambayo yalihitaji afanyiwe upasuaji ambao ungemuweka nje kwa zaidi ya wiki tatu, hivyo akapewa ruhusa ya kuondoka kwenye kambi.

Badala ya kwenda kufanyiwa upasuaji kama ilivyotarajiwa katika hali isiyokuwa ya kawaida jana ambapo ilikuwa ni wiki moja tangu adaiwe kupata majeraha hayo, staa huyu alionekana kwenye mchezo huo.

Kocha wa Nigeria Jose Peseiro alipoulizwa kuhusiana na tukio hilo alisema ameshangazwa kwa sababu alipokea ripoti kutoka kwa madaktari wa timu ambao walimwambia kwamba staa huyo hatoweza kurudi kwenye hali yake na alihitaji walau siku 14.