Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Spurs yaweka rekodi mbovu

Muktasari:

  • Miamba hiyo ya London Kaskazini ilikumbana na kichapo kutoka kwa Leicester City ikiwa ni mwendelezo wa matokeo mabaya kwao msimu huu.

LONDON, ENGLAND: TOTTENHAM Hotspur imevunja rekodi ya hovyo zaidi iliyodumu kwa zaidi ya muongo mmoja baada ya kuchapwa na Leicester City kwenye Ligi Kuu England.

Miamba hiyo ya London Kaskazini ilikumbana na kichapo kutoka kwa Leicester City ikiwa ni mwendelezo wa matokeo mabaya kwao msimu huu.

Spurs ilitangulia kufunga kwenye dakika ya 33 kupitia kwa fowadi Richarlison. Lakini, dakika tano tu baada ya kuanza kipindi cha pili, timu hiyo ya kocha Ange Postcoglou ilijikuta ikipoteza mchezo wakati Jamie Vardy alipofunga bao la kusawazisha na Bilal El Khannouss akafunga la ushindi.

Hiyo ilikuwa mara ya kwanza kwa Spurs kuruhusu wavu kuguswa mara mbili ndani ya dakika tano za mwanzo kwenye kipindi cha pili kwenye Ligi Kuu tangu Novemba 1987 dhidi ya Liverpool. Leicester City iliingia kwenye mechi hiyo ikiwa kama timu kibonde baada ya kupoteza katika mechi saba zilizopita kwenye Ligi Kuu England. Kipigo hicho ina maana Spurs imepoteza kwa timu yenye rekodi kama hiyo kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1912, miaka 113 iliyopita.

Kipindi hicho Spurs ilifungwa na Notts County. Kipigo kinaiacha Spurs kwenye nafasi ya 15 katika msimamo, pointi nane juu ya timu tatu za chini.

Spurs haijashinda kwenye mechi saba zilizopita, ikipoteza sina na kutoka sare moja. Na hiyo ni mechi nyingi kwa timu hiyo tangu ilipokaa kwa mechi tisa bila ya kushinda kati ya Mei na Oktoba 2008. Hiyo ina maana Spurs imepoteza mechi 13 kati ya 23 ilizocheza kwenye Ligi Kuu England, ikishinda saba na sare tatu. Baada ya kichapo, kocha Postcoglou alisifu wachezaji kwa kucheza kwa jitihada zote.

Alisema: “Ni matokeo ya kuhuzunisha, lakini muda huo huo siwezi kuhitaji ziada kutoka kwa wachezaji wangu. Wamejitahidi kwa nguvu zote, lakini mambo tu yameshindwa kwenda kombo upande wetu. Tulikuwa na nafasi ya kumaliza mechi, lakini hatukufanya hivyo.”