Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Spurs wanamtaka Pochettino

LONDOM, ENGLAND. TOTTENHAM Hotspur imeripotiwa kuwa na mpango wa kumrudisha kocha Mauricio Pochettino kwenye kikosi chake mwishoni mwa msimu huu ili apige mzigo kuanzia msimu ujao.

Juzi Jumapili, Spurs iliichapa West Ham United mabao 2-0 katika mchezo wa Ligi Kuu England na hivyo kuingia kwenye Top Four ya ligi hiyo, wakijaribu kusaka nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Hata hivyo, matokeo hayo yamekuja wakati Cristian Stellini akiwa kwenye benchi la ufundi baada ya kocha mkuu wa kikosi hicho, Antonio Conte kuwa nje kutokana na kufanyiwa upasuaji hivi karibuni.

Wakati Conte akitarajiwa kurejea uwanjani wakati atakapokuwa sawa kiafya, mabosi wa Spurs wameshaanza kufikiria kitu watakachofanya mwishoni mwa msimu huu kwenye ishu ya kocha. Spurs watakuwa na shughuli pevu pia ya kuhakikisha straika wao, Harry Kane anaendelea kubaki kwenye kikosi hicho hadi msimu ujao.

Kwa mujibu wa mwandishi Nicolo Schira, mabosi wa Spurs wanafikiria kumrudisha Pochettino kwenye benchi la ufundi la timu hiyo. Muargentina huyo aliwahi kuwa kocha wa Spurs kati ya Mei 2014 na Novemba 2019, akishinda mechi 159 kati ya 293 alizoisimamia timu hiyo na aliwafikisha fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Tangu Pochettino alipoondoka Spurs, timu hiyo imebadilisha makocha mara tatu, walianza na Jose Mourinho, Nuno Espirito Santo na sasa Conte. Taarifa nyingine zinadai Pochettino yupo kwenye rada za Atletico Madrid.