Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Spurs mnalo hilo, Bukayo Saka anarudi

SAKA Pict

Muktasari:

  • Winga huyo wa Arsenal alipata jeraha la misuli, linaloaminika kuwa karibu na eneo la nyonga, wakati wa mazoezi ya awali kabla ya miamba hiyo ya Emirates kuichapa Leeds United mabao 4-0, Jumamosi iliyopita.

LONDON, ENGLAND: BUKAYO Saka analenga kurejea uwanjani akiwa fiti kwa ajili ya dabi ya North London itakayochezwa baadaye mwezi huu.

Winga huyo wa Arsenal alipata jeraha la misuli, linaloaminika kuwa karibu na eneo la nyonga, wakati wa mazoezi ya awali kabla ya miamba hiyo ya Emirates kuichapa Leeds United mabao 4-0, Jumamosi iliyopita.

Saka sasa anakabiliwa na kipindi cha kukaa nje ya uwanja na alikosa mechi ya Jumanne ya marudiano ya nusu fainali ya Kombe la Carabao dhidi ya Chelsea, ambapo Arsenal ilishinda 1-0 na hivyo kutinga fainali kwa kishindo cha jumla ya mabao 4-2 kufuatia matokeo ya 3-2 katika mechi ya kwanza.

Hata hivyo, jeraha hilo si kubwa na matumaini ni kwamba Saka atakuwa fiti wakati Arsenal itakapoifuata Tottenham, Februari 22.

Nyota huyo wa kimataifa wa England ana hamu kubwa ya kurejea haraka iwezekanavyo na anaweza hata kurejea mapema zaidi iwapo mpango wake wa kurekebisha hali ya mwili utaenda vizuri.

Arsenal ina ratiba nyepesi kabla ya mechi dhidi ya Spurs kwa kuwa haishiriki michezo ya mchujo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwezi huu. Baada ya mchezo dhidi ya Chelsea, kikosi cha Mikel Arteta kitaikaribisha Sunderland katika Ligi Kuu England, Jumamosi kabla ya kusafiri kwenda Brentford, Alhamisi ijayo.

Baadaye, Arsenal itaialika Wigan kwenye Uwanja wa Emirates, Jumapili inayofuata katika Raundi ya Nne ya Kombe la FA.

Saka analenga kurejea uwanjani wiki inayofuata, ambapo Arsenal itasafiri kwenda Wolves katikati ya wiki na kabla ya kuitembelea Tottenham, Jumapili.

Noni Madueke ndiye anayebeba jukumu la kuziba pengo lililoachwa wazi na Saka. Madueke alionyesha kiwango kizuri dhidi ya Leeds United wikendi iliyopita alipoingizwa kikosini dakika za mwisho kabla ya mechi kuanza. Alitoa pasi ya goli la kwanza kisha akafunga bao la pili moja kwa moja kwa mpira wa kona aliyochonga.