Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Spurs ilivyobaki EPL kwa Mbinde

SPURS Pict

Muktasari:

  • Awali, ushindi wa West Ham United wa mabao 3-0 dhidi ya Leeds United ulimaanisha Spurs wangeshuka daraja iwapo wangepoteza mchezo huo, lakini Everton hawakuonyesha maajabu ya kukipa changamoto zozote kikosi hicho cha kocha Roberto De Zerbi.

LONDON, ENGLAND: MSIMU wa Ligi Kuu England ulimalizika mwishoni mwa wiki ukiwa na furaha kubwa kwa Tottenham Hotspur baada ya bao la Joao Palhinha kuipa ushindi muhimu nyumbani na kuiepusha kushuka daraja siku ya mwisho ya msimu kwa  kuifunga Everton bao 1-0.

Awali, ushindi wa West Ham United wa mabao 3-0 dhidi ya Leeds United ulimaanisha Spurs wangeshuka daraja iwapo wangepoteza mchezo huo, lakini Everton hawakuonyesha maajabu ya kukipa changamoto zozote kikosi hicho cha kocha Roberto De Zerbi.

Spurs walianza mchezo kwa kasi wakisukumwa na mashabiki waliokuwa na hamasa kubwa katika Uwanja wa Tottenham Hotspur, huku Conor Gallagher na Kevin Danso wakikosa nafasi za mapema za kufunga. Hata hivyo, mchezo ulianza kupungua kasi kabla ya dakika ya 43 ambapo bao la ushindi lilipatikana kupitia Palinha.

Everton walionekana dhaifu kwenye ushambuliaji, na ilikuwa hadi dakika za nyongeza ndipo walipopata shuti la kwanza lililolenga lango, kupitia Tyrique George aliyemlazimisha kipa Antonin Kinsky kufanya sevu muhimu. Ushindi huo ulikuwa wa kwanza wa nyumbani kwa Spurs katika ligi tangu Desemba na uliwahakikishia kuendelea kubaki Ligi Kuu England msimu ujao.

SPU 01

SPURS KWA MBINDE EPL

Uchambuzi wa takwimu unaonyesha kwamba, Arsenal pekee ndio waliokuwa na rekodi ya mabao 19 ya kona 2025-26 kuliko Tottenham waliofunga 18. Hivyo ilikuwa sahihi kuona bao lao la ushindi likitokana na kona. Ingawa Spurs wanaweza kusherehekea kubaki ni lazima waboreshe kiwango msimu ujao.

Huo ulikuwa ushindi wao wa tatu pekee wa nyumbani msimu huu, idadi inayolingana na rekodi ya ushindi mara chache zaidi nyumbani kwa timu iliyosalia Ligi Kuu England sambamba na Hull City msimu wa 2008-09.

Kwa upande wa Everton, wamehitimisha msimu uliotarajiwa kuwa wa maendeleo wakiwa nafasi ileile waliyomaliza msimu uliopita tofauti ikiwa ni pointi moja zaidi. Everton hawajashinda katika mechi saba za mwisho za ligi hiyo wakiwa na sare tatu pamoja na vipigo vinne, rekodi inayolingana na kipindi kibaya zaidi bila ushindi chini ya kocha David Moyes.

Lakini, mchezo huo ulikuwa na mashuti matatu pekee yaliyolenga lango, Spurs wakiwa na mawili huku Everton wakipata moja.

SPU 03

MIAKA 14 WEST HAM EPL

Juzi, takwimu mbalimbali za kimichezo Ulaya ziliipa West Ham United nafasi kubwa ya kushuka daraja katika siku ya mwisho. Na licha ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Leeds United, Hammers watacheza Championship msimu ujao.

West Ham United walishuka daraja kutoka Ligi Kuu England kwa mara ya kwanza baada ya miaka 14, na kikosi hicho kilichokuwa chini ya kocha Nuno Espírito Santo kiliingia katika mchezo wa mwisho wa msimu kikijua lazima kishinde ili kiwe na nafasi ya kubaki kazi ambayo kiliifanya kwa ufasaha.  Hata hivyo, kutokana na tofauti ya mabao, matumaini yake yalitegemea pia Tottenham kufungwa na Everton suala ambalo halikutokea.

SPU 05

Kulikuwa na hali ya kukata tamaa kipindi cha kwanza baada ya West Ham kushindwa kutengeneza nafasi nyingi za wazi, na Leeds walionekana kuwa karibu zaidi kufunga kupitia Lukas Nmecha na Dominic Calvert-Lewin, huku taarifa zikienea kuwa Palhinha alikuwa ameifungia Spurs bao la kuongoza.

West Ham walipambana kipindi cha pili, ambapo Valentin Castellanos alifunga kwa kichwa baada ya kona kutoka kwa Jarrod Bowen dakika ya 67. Bowen mwenyewe aliongeza bao la pili dakika ya 79 baada ya Pascal Struijk kushindwa kuzuia pasi ya Mateus Fernandes na mchezaji aliyeingia kipindi cha pili Callum Wilson alifunga bao la tatu kwa shuti kali dakika za nyongeza.

West Ham wameshuka kwa kwanza tangu msimu wa 2010-11, licha ya kukusanya pointi 39. Hiyo ndiyo idadi kubwa zaidi ya pointi kwa timu iliyoshuka daraja tangu Birmingham City na Blackpool zishuke zikiwa na pointi 39 msimu wa 2010-11.

SPU 04

Ingawa kupoteza mechi tatu mfululizo kabla ya siku ya mwisho kuligharimu timu hiyo, West Ham pia ilikuwa na mwanzo mbaya wa msimu ulioiweka kwenye vita ngumu ya kusalia Ligi Kuu England, lakini kama matokeo ya mechi tangu siku ya kwanza ya Nuno kuinoa Septemba 29, 2025 pekee ndiyo yangehesabiwa, West Ham ingemaliza nafasi ya 16 ikiwa na pointi 36 kwani ameshinda mara tisa, sare tisa na vipigo 15.

Kinachobaki sasa inabaki ni kama baadhi ya nyota wataondoka baada ya kushuka daraja akiwa nahodha Jarrod Bowen anayetarajiwa kuvutia klabu nyingi baada ya kumaliza msimu akiwa na asisti 11 ikiwa ni rekodi yake bora zaidi katika msimu mmoja akihusika na jumla ya mabao 20.

Ni Paolo Di Canio 1999-00 aliyekuwa na asisti 13 na Dimitri Payet 2015-16 (12) pekee waliohusika nazo nyingi zaidi kwa West Ham katika msimu mmoja wa ligi hiyo. Kushuka kwa West Ham kunahitimisha timu tano ambapo inaungana na Wolverhamton Wandereres na Burnley.

Wolves ilikuwa timu ya kwanza kushuka daraja msimu huu zikiwa bado mechi tano kuchezwa. Katika siku zote 282 za msimu wa 2025-26, Wolves walikuwa ndani ya eneo la kushuka daraja. Hivyo wakawa timu ya kwanza kutumia asilimia 100 ya siku za msimu mzima ndani ya mstari wa kushuka tangu wao wenyewe walipofanya hivyo 1964-65, walipokuwa katika nafasi za kushuka kwa siku zote 250.

SPU 02

Timu zilizoshuka Ligi Kuu England mara nyingi zaidi tangu msimu wa 1992/1993 ni Norwich City mara sita; West Bromwich, Leicester City na Burnley kila moja mara tano; Middlesbrough, Sheffield United, Watford na Sunderland mara nne kila moja, huku Birmingham City, Bolton Wanderers, Crystal Palace, Fulham, Hull City, Nottingham Forest, Queens Park Rangers, Southampton, Ipswich Town, West Ham United, na Wolverhampton Wanderers mara tatu tatu.

Zingine ni Blackburn Rovers, Cardiff City, Charlton Athletic, Derby County, Leeds United, Manchester City, Newcastle United na Reading zilizoshuka mara mbilimbili huku Aston Villa, Barnsley, Blackpool, Bournemouth, Bradford City, Coventry City, Huddersfield Town, Oldham Athletic, Portsmouth, Sheffield Wednesday, Stoke City, Swansea City, Swindon Town, Wigan Athletic, Wimbledon na Luton Town kila moja ikishuka Championship mara moja moja.


ZIMEPANDA EPL 2026/27

  • Coventry City
  • Hull City
  • Ipswich Town