Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Spurs, West Ham nani kubaki EPL?

Muktasari:

  • Lakini, hadi siku ya mwisho ya msimu ambayo inahitimishwa leo, Jumapili, bado kuna timu moja inayopaswa kuungana na hizo mbili ili kucheza Championship msimu ujao.

LONDON, ENGLAND: MBIO za ubingwa wa Ligi Kuu England zimekwisha baada ya Arsenal kubeba wiki iliyopita, lakini vita vya kushuka daraja bado vibichi baada ya Burnley kuhitimisha msimu wake mmoja katika mashindano hayo na na Wolverhampton Wanderers iliyoitangulia kuachia ngazi.

Lakini, hadi siku ya mwisho ya msimu ambayo inahitimishwa leo, Jumapili, bado kuna timu moja inayopaswa kuungana na hizo mbili ili kucheza Championship msimu ujao.

Macho yote kwa sasa yanaelekezwa kwa wapinzani wa jadi wa London, Tottenham Hotspur na West Ham United ambao wanaingia katika mechi ya mwisho ya msimu wakijua kwamba mmoja atasalia Ligi Kuu Enngland huku mwingine akishuka daraja.

Tottenham wanaonekana kuwa katika nafasi nzuri zaidi kutokana na tofauti ya pointi mbili walizo nazo dhidi ya West Ham na hilo lina maana kuwa ushindi dhidi ya Everton utawahakikishia kubaki katika michuano hiyo bila kujali matokeo ya West Ham United.

Hata sare inaweza kuwatosha Spurs kutokana na kuwa na tofauti bora ya mabao. Lakini wakifungwa, mlango utafunguka kwa West Ham ambao nao wanapaswa kwanza kuifunga Leeds United ili kuwa na matumaini ya kupona.

HISTORIA INASEMAJE?

Katika historia ya Ligi Kuu England vita vya kushuka daraja mara nyingi huamuliwa siku ya mwisho ya msimu, ambapo kati ya misimu 34, huu ni  wa 24 ambapo angalau timu moja inayoshuka daraja itajulikana siku ya mwisho.

Kwa kawaida, timu zinazoanza siku ya mwisho zikiwa ndani ya eneo la kushuka daraja huishia kushuka, na hilo limetokea mara 14. Lakini bado kuna matumaini kwa West Ham, kwani katika misimu tisa, timu iliyokuwa kwenye mstari wa kushuka daraja ilifanikiwa kujinasua siku ya mwisho. Hata hivyo, imekuwa nadra sana katika miaka ya karibuni. Tangu 2011, ni mara moja tu ambapo timu imefanikiwa kutoka kwenye mstari wa kushuka daraja siku ya mwisho pale Leeds United walipojinasua 2021-22 kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Brentford na kuipeleka Burnley hadi Championship. Kwa hiyo, historia ya karibuni inaonyesha kuwa kazi inayowasubiri West Ham ni ngumu sana.


FOMU YA TIMU

Cha kushangaza ni kwamba, licha ya timu hizo kuwa katika hatari ya kushuka daraja, kiwango chao cha karibuni siyo kibaya sana, kwani Spurs wameonekana kuimarika tangu kuwasili kwa kocha Roberto De Zerbi na kabla ya kufungwa na Chelsea katikati ya wiki walikuwa hawajapoteza mechi nne mfululizo.

Kwa upande wa West Ham, licha ya kuwa katika mfululizo wa vipigo vitatu, wamekuwa imara sana wanapocheza nyumbani. Kabla ya kufungwa na mabingwa, Arsenal, walikuwa hawajapoteza nyumbani tangu Januari. Hilo lina maana kuwa wana sababu ya kuamini wanaweza kuifunga Leeds wikendi hii.

Tatizo kubwa kwa Spurs ni rekodi mbaya nyumbani. Katika msimu mzima  wameshinda mechi mbili nyumbani, na hakuna ushindi wowote tangu Desemba. Hali hiyo imeendelea hata chini ya De Zerbi. Mara kadhaa wamekuwa wakiongoza lakini wakashindwa kulinda ushindi.


TOTTENHAM NA HOFU YA MASHABIKI

Katika soka la England kuna msemo maarufu unaoitwa “Dk Tottenham†. Huo ni utani unaomaanisha kuwa Spurs huwa timu inayosaidia wapinzani kumaliza vipindi vibaya vya matokeo. Kwa mfano, msimu huu wamevunja rekodi za timu nne zilizokuwa hazijashinda kwa muda mrefu ikiwemo Bournemouth, Chelsea, West Ham na Nottingham Forest.

Kutokana na historia hiyo, mashabiki wa Spurs wana hofu kubwa kwamba wanaweza tena kuwasaidia Everton kumaliza kipindi chao kibaya.

Presha kutoka kwa mashabiki zaidi ya 60,000 ndani ya Uwanja wa Tottenham Hotspur inaweza kuwa mzigo mkubwa kwa wachezaji wao.

Kwa upande wa West Ham, nao wanakutana na Leeds walio katika kiwango bora wakiwa hawajapoteza mechi nane mfululizo.


KOMPYUTA YA UTABIRI INASEMAJE?

Kwa mujibu wa kopyuta maalumu ya utabiri ‘Opta Supercomputer’, mambo yanaonekana mabaya zaidi kwa West Ham United ikitabiri kwamba  wana uhakika wa kushuka daraja kwa asilimia 85.5, huku Spurs wakiwa na 14.5. Sababu kubwa ni kwamba Spurs wana nafasi kubwa zaidi ya kupata matokeo dhidi ya Everton kuliko West Ham walivyo dhidi ya Leeds.

Kwa mujibu wa viwango vya Opta, Tottenham ni timu ya 32 duniani, Everton 24, West Ham 43 na Leeds inakamata nafasi ya 25. Hivyo, Spurs wanaonekana kuwa karibu zaidi kwa ubora na wapinzani wao kuliko West Ham walivyo.

Lakini mpira una hisia na tatizo ambalo kompyuta haiwezi kulipima ni hisia za kibinadamu. Haiwezi kuelewa presha ya mashabiki, hofu ya kushuka daraja au namna akili ya mchezaji inaweza kubadilika katika mechi kubwa. Spurs wanaweza kuingia uwanjani wakijaribu kulinda sare badala ya kushinda, jambo ambalo linaweza kuwa hatari sana.

West Ham nao wanaweza kutumia nguvu ya mashabiki wao wa nyumbani kupata ushindi muhimu. Kwa hiyo, licha ya Tottenham kuwa katika nafasi nzuri zaidi, vita vya kushuka daraja bado iko wazi.