Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Solanke afunga bao la kideo kama Giroud

SOLANKE Pict

Muktasari:

  • Mchezaji huyo wa timu ya taifa ya England alifunga staili ya mapigo ya mpira yanayofahamika kama “scorpion kick” , inayofanana na ile ya Olivier Giroud, na kufanya matokeo kuwa 2-2 katika Uwanja wa Tottenham Hotspur.

LONDON, ENGLAND: STRAIKA Dominic Solanke huenda amefunga bao la msimu baada ya kusawazisha kwa njia ya ubunifu wa hali ya juu dhidi ya Manchester City.

Mchezaji huyo wa timu ya taifa ya England alifunga staili ya mapigo ya mpira yanayofahamika kama “scorpion kick” , inayofanana na ile ya Olivier Giroud, na kufanya matokeo kuwa 2-2 katika Uwanja wa Tottenham Hotspur.

Conor Gallagher alifanya kazi ya ajabu kwa kuupora mpira Man City waliokuwa wametulia upande wa kulia na kuanzisha shambulizi.

Nyota huyo wa zamani wa Chelsea kisha alipiga krosi ndani ya boksi, na licha ya mpira kuwa nyuma ya Solanke, mshambuliaji huyo aliweza kuupiga kwa staili hiyo ya scorpion kick na kuutuma nyavuni.

Jaribio hilo lilikuwa la kushangaza na lisilotarajiwa kiasi kwamba kipimo cha matarajio ya bao (xG) kilimpa Solanke nafasi ya asilimia 4 tu (0.04) ya kufunga.

Solanke alikuwa amerudi hivi karibuni katika kikosi cha Spurs baada ya kipindi kigumu cha majeraha, lakini mabao yake mawili yaliwasaidia kurejea mchezoni dhidi ya Man City inayowania ubingwa na kuambulia sare ya 2-2. Kwa kushangaza, mabao yake ya staa wa Spurs yanaonekana kuisaidia Arsenal kudumisha uongozi wa pointi sita kileleni mwa Ligi Kuu England.

Wachambuzi wa Sky Sports walibaki vinywa wazi wakati mpira uliopigwa na Solanke ulipopaa juu ya kipa Gianluigi Donnarumma na kuingia kwenye lango la Man City. Gary Neville amesema: “Mpira uko nyuma yake… atawahi kufunga bao bora kuliko hilo? Sidhani. Hilo litakuwa juu kabisa. “Huenda si bora kama lile nililoliona Emirates miaka iliyopita. (Olivier) Giroud alikuwa mbali zaidi.”

Aliongeza: “Hatafunga tena bao kama hilo katika maisha yake ya soka.”

Mchezaji huyo aliyesajiliwa kwa Pauni 60 milioni ameiongoza Spurs kurejea kwa nguvu kipindi cha pili baada ya kuonekana dhaifu wakiwa nyuma kwa mabao 2-0. Akiwa karibu kutimiza hat-trick, Solanke alitolewa nje katika dakika za majeruhi baada ya kuumia kifundo cha mguu, lakini mshambuliaji huyo amesisitiza kuwa jeraha hilo si kubwa.