Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Slot: Wote macho kwa Mo Salah

Muktasari:

  • Na kocha huyo Mdachi amewaonya wachezaji wake kwamba kushuka kiwango kwa asilimia moja tu kutakuwa na athari kubwa kwenye mipango ya kunyakua ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu.

LIVERPOOL, ENGLAND: KOCHA wa Liverpool, Arne Slot anasema anaamini kila mchezaji wa timu hiyo anapaswa kufikia kwenye viwango vya supastaa Mohamed Salah.

Na kocha huyo Mdachi amewaonya wachezaji wake kwamba kushuka kiwango kwa asilimia moja tu kutakuwa na athari kubwa kwenye mipango ya kunyakua ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu.

 Kikosi hicho cha Slot kilikuwa na kasheshe usiku wa Jumatano wa kumenyana na Newcastle United katika michuano ya Ligi Kuu England.

Liverpool inachokiona ni kama vile imeshaweka mkono mmoja kwenye taji hilo na ilikuwa na matumaini ya kuendelea kuwa na pengo la pointi kileleni kwenye msimamo wa ligi hiyo. Na ujumbe wa kocha huyo kwa wachezaji wake, kwamba wanapaswa kumtazama Mo Salah kutokana na kiwango cha juu anachocheza kuhakikisha timu inanyakua taji la Ligi Kuu England.

Slot alisema: “Kama unataka kucheza kwenye hii timu basi unahitaji kuwa kwenye kiwango cha juu sana vinginevyo utaishia kuona wengine tu wanaocheza kwenye ubora wa juu wakipata nafasi. Kwa sababu hii ni moja ya timu bora kama sio bora kabisa duniani kuichezea.”

Salah amehusika kwenye mabao 51 kabla ya mechi ya Newcastle United, akifunga 30 na kuasisti 21. Amekuwa mchezaji wa kwanza kwenye Ligi Kuu England kufunga mabao 25 na kuasisti mara 15 msimu mmoja. Na kitu cha ziada alichoonyesha kwenye kikosi ni juu ya kushiriki kwenye kukaba pia.

Slot alisema: “Sio ishu ya matokeo, hii inahusu jitihada unazoweka. Huwezi kumiliki matukio yanayoweza kutokea kama lile la dakika 97 dhidi ya Everton. Lakini, unachopaswa kufanya ni kupambana.”