Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tottenham yatakiwa kuvunja benki kumsajili Marcus Rashford

Muktasari:

  • Man United wanataka kupunguza mzigo wa mishahara na wako tayari kumruhusu aondoke kwa Dau la karibu Pauni 30 milioni. Rashford, bado ana mkataba Old Trafford na hana mpango wa kurudi klabuni hapo.

Kiungo wa zamani wa Tottenham, Jamie O’Hara ameiomba klabu hiyo ‘ivunje benki’ kumsajili mshambuliaji wa Manchester United, Marcus Rashford. O’Hara anadai Rashford ni nyota muhimu kutua Tottenham chini ya Roberto De Zerbi.

Man United wanataka kupunguza mzigo wa mishahara na wako tayari kumruhusu aondoke kwa Dau la karibu Pauni 30 milioni. Rashford, bado ana mkataba Old Trafford na hana mpango wa kurudi klabuni hapo.


Yan Diomande

Yan Diomande ameweka wazi mwelekeo wake wa baadaye baada ya kuibuka kuwa amependelea kujiunga na Paris Saint-Germain endapo ataondoka RB Leipzig, hatua inayoripotiwa kuipiga pigo kubwa Liverpool waliokuwa tayari kutoa karibu Euro 100 milioni. Inadaiwa Diomande anaamini mfumo wa PSG chini ya Luis Enrique ni bora zaidi kwake kuendeleza ndoto za kushinda mataji makubwa na baadaye kuwania tuzo ya Ballon d’Or.


Bruno Guimarães

Arsenal inataka kurudi tena na ofa nzuri baada ya ile ya awali ya Pauni 55 milioni kukataliwa na Newcastle United kwa ajili ya kiungo Bruno Guimarães. Kocha Mikel Arteta anamwona nyota huyo wa Brazil kama kiungo muhimu wa kuimarisha umiliki wa mpira. Newcastle United bado wanapanga kumlinda nahodha wao aliye na mkataba hadi mwaka 2028 licha ya presha ya timu zinazomtaka.


Endrick

MSHAMBULIAJI Endrick amepewa nafasi ya kurejea kwenye kikosi cha Real Mdrid moja kwa moja baada ya klabu hiyo na Kocha Jose Mourinho kukubaliana kumtumia msimu ujao baada ya mkataba wake wa mkopo kumalizika Lyon ya Ufaransa. Nyota huyo wa Brazil atabaki Santiago Bernabéu kuanza msimu mpya chini ya Mourinho, huku akitarajiwa kupigania nafasi kikosini baada ya uzoefu wake Lyon.


Malo Gusto

Malo Gusto amekubali masharti binafsi ya kujiunga na Manchester City kutoka Chelsea dirisha la majira ya kiangazi. Beki huyo wa kulia wa Ufaransa anatajwa kuvutiwa na uwezekano wa kufanya kazi tena na kocha wake wa zamani, Enzo Maresca, ambaye anahusishwa na mipango ya kikosi kipya Etihad. Mazungumzo kati ya klabu hizo mbili bado yanaendelea kuhusu ada ya uhamisho.


Granit Xhaka

Chelsea imepata pigo katika mipango yao ya usajili baada ya Sunderland kukataa ofa ya awali ya kumsajili kiungo Granit Xhaka na mchezaji huyo si wa kuuzwa kwa gharama yoyote. Inadaiwa Chelsea walitoa ofa ya Pauni 8 milioni ili kumrejesha Xhaka kufanya kazi tena na kocha Xabi Alonso, lakini Sunderland wameweka msimamo mkali wa kumbakiza nahodha wao.


Mateus Fernandes

Manchester United na Tottenham Hotspur wameingia kwenye mbio kali za kumsajili kiungo Mateus Fernandes anayekipiga West Ham United, huku mazungumzo ya awali yakiwa tayari yameanza kati ya pande zote.

Inadaiwa timu hizo zinamfuatilia kwa karibu kiungo huyo wa Ureno, lakini West Ham wanashikilia msimamo mkali wa kutomuuza kwa bei ya chini.