Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Slot: Salah ni Cristiano Ronaldo mtupu

Slot Pict

Muktasari:

  • Salah ambaye amecheza karibia mechi 700 katika maisha yake ya soka hadi sasa, msimu huu amefunga mabao 27 katika michuano yote akiisaidia Liverpool kuongoza katika msimamo wa ligi pia.

LIVERPOOL, ENGLAND: AKIWA na umri wa miaka 32 kwa sasa, staa wa Liverpool, Mohamed Salah au King Salah kama anavyoitwa na mashabiki wake, amemkosha sana kocha wake Arne Slot ambaye anadai utimamu wa mwili wa fundi huyu ni sawa na Cristiano Ronaldo.

Salah ambaye amecheza karibia mechi 700 katika maisha yake ya soka hadi sasa, msimu huu amefunga mabao 27 katika michuano yote akiisaidia Liverpool kuongoza katika msimamo wa ligi pia.

“Umri wake unadhihirisha kile anachokionyesha uwanjani, ni mtaalamu sana na mwerevu sana na anajua vizuri sana wapi mpira utaanguka, ameshapitia mengi katika soka kiasi na anajua tu mahali mpira utakapoanguka na huwa anakaa eneo hilo  kama alivyofanya alipoifungia Everton Jumatano,” alisema Slot na kuongeza,

“Katika maeneo mengine, kama vile jinsi alivyo na mwili mzuri, ana uwezo wa kucheza kila baada ya siku tatu kwa umri wake  ingawa sio peke yake, nafikiri Cristiano Ronaldo bado anafanya hivyo akiwa na umri wa miaka 40, lakini Mo  ni mfano mzuri kwa wachezaji wetu vijana.”

“Ana uwezo wa kuonyesha kiwango chake bora kila baada ya siku chache. Miaka 32 siyo mingi sana kwa mchezaji wa soka bado ni umri mzuri kuwa nao, nafikiri.”

Salah anamaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu huu na imeendelea kuripotiwa  msimu huu unaweza kuwa  wa mwisho kwake katika timu hiyo.

Slot anaamini staa huyu ana uwezo wa kucheza kwa muda mrefu na kiwango bora zaidi na ikiwa atasainishwa mkataba mpya utapaswa kuwa wa muda mrefu tofauti na miaka miwili kama inavyotajwa.

“Kile kinachonivutia zaidi ni Mo ni mtu mnyenyekevu sana anayetaka kufanya kazi kila siku ili kuwa mchezaji bora,” aliongeza Slot.

Kabla ya mchezo wa jana dhidi ya Wolves, Salah  alikuwa amefunga katika michezo yake mitano iliyopita Anfield.