Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Slot aweka wazi hatma ya Ibrahima Konate

KONATE Pict

Muktasari:

  • Konate amekuwa akihusishwa na uwezekano wa kujiunga na Real Madrid kwa uhamisho wa bure mwishoni mwa msimu, lakini Slot ameweka wazi kuwa bado anataka Mfaransa huyo abaki na kusaini mkataba mpya.

LIVERPOOL, ENGLAND: KOCHA wa Liverpool, Arne Slot, amefunguka kuhusu mustakabali wa beki kisiki wa timu hiyo raia wa Ufaransa, Ibrahima Konate ambaye mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu.

Konate amekuwa akihusishwa na uwezekano wa kujiunga na Real Madrid kwa uhamisho wa bure mwishoni mwa msimu, lakini Slot ameweka wazi kuwa bado anataka Mfaransa huyo abaki na kusaini mkataba mpya.

Hatma ya Konate bado haijawa wazi wakati huu ambapo amebakisha muda mchache katika mkataba wake.

Beki huyo alianza vibaya msimu huu, lakini amerejea katika kiwango kizuri hivi karibuni tangu aliporudi baada ya mapumziko ya msiba kufuatia kifo cha baba yake.

Konate alifunga bao alipopata nafasi ya kurejea tena kiwanjani dhidi ya Newcastle, lakini alikiri kuwa ilikuwa kipindi kigumu kwake na familia yake kutokana na msiba walioupata.

Akizungumza na TNT Sports, amesema: "Kwa hakika nina furaha sana, na sina maneno ya kueleza ninavyojisikia hivi sasa, kwa sababu ilikuwa kipindi kigumu sana kwa familia yangu na kwangu katika wiki mbili zilizopita. Hii ni sehemu ya maisha. Ni vigumu kukubali, lakini hatuna namna nyingine."

"Niliona timu ilikuwa na wachezaji wengi majeruhi. Kocha alinipigia simu akaniambia nipumzike kadri nitakavyohitaji, sina haja ya kuharakisha kurejea. Lakini binafsi nilihisi ilikuwa muhimu nirejee na kusaidia timu. Nafikiri ndivyo nilivyofanya leo."

Awali, Konaté alionekana kama angetimkia Madrid, lakini Los Blancos waliripotiwa kuachana na mpango wa kumsajili mapema msimu huu kutokana na kushuka kwa kiwango chake.

"Tuko kwenye mazungumzo naye, hiyo inatosha kuonyesha tunachohitaji. Ni wazi tungependa abaki, lakini mazungumzo bado yanaendelea, kwa hiyo tusubiri tuone yataishia wapi. Tusingeanzisha mazungumzo kama tusingehitaji kumbakisha."

“Konate amekuwa katika kipindi kizuri sana hivi karibuni. Alikuwa na michezo mingi mizuri mwanzoni mwa msimu, lakini pia kulikuwa na nyakati ambapo makosa madogo aliyofanya yalisababisha sisi kufungwa bao, hivyo akahukumiwa na mashabiki kwa makosa hayo. Kwa ujumla kiwango chake kilikuwa kizuri."