Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sir Jim Ratcliffe: Mabadiliko yameanza kuzaa matunda

TAJIRI Pict

Muktasari:

  • Man United ilipitia msimu mbaya zaidi katika kipindi cha miaka 51 iliyopita, ilipomaliza katika nafasi ya 15 kwenye Ligi Kuu ya England msimu uliopita na kushindwa kutwaa taji lolote.

MANCHESTER, ENGLAND: TAJIRI wa Manchester United, Sir Jim Ratcliffe amesema kuwa baadhi ya maamuzi aliyoyafanya ndani ya Manchester United yanaanza “kuzaa matunda”.

Ratcliffe anatimiza miaka miwili ya uongozi wake mwishoni mwa mwezi huu tangu anunue sehemu ya hisa ya klabu hiyo mwaka 2024.

Katika kipindi hicho, Man United imepunguza wafanyakazi takribani theluthi moja, wameongeza bei za tiketi, na wamewafukuza makocha wawili.

Man United ilipitia msimu mbaya zaidi katika kipindi cha miaka 51 iliyopita, ilipomaliza katika nafasi ya 15 kwenye Ligi Kuu ya England msimu uliopita na kushindwa kutwaa taji lolote.

Msimu huu ina dalili zote za kumaliza bila ya kutwaa taji lolote ingawa iko nafasi ya nne baada ya kushinda mechi nne mfululizo tangu Michael Carrick achukue mikoba ya kuinoa kama kocha wa mpito baada ya kufukuzwa kwa Ruben Amorim.

Mkataba wa Carrick na Man United unamalizika mwishoni mwa msimu, na kwa sasa mashetani hao wameendelea na mchakato wa kumtafuta kocha mpya wa kudumu.

Mkurugenzi wa Ineos, Ratcliffe, ambaye amekuwa akikabiliwa na ukosoaji mkubwa kutoka kwa mashabiki wa Man United amekiri kuwa amekuwa anajua kwamba hawafurahishi mashabiki, lakini yeye anafanya yote kwa ajili ya timu.

“Najua nimekuwa siwafurahishi sana mashabiki wa Manchester United kwa sababu ya kufanya mabadiliko mengi. Lakini kwa mtazamo wangu, ni kwa ajili ya kuijenga Man United.”