Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Magwiji Man United watofautiana kuhusu Carrick

Muktasari:

  • Lengo lilikuwa Carrick aisaidie klabu kurejesha utulivu kabla ya kuondoka na kumpisha kocha mwenye jina kubwa zaidi. Hata hivyo, Carrick amezidi matarajio hayo kwa kuiongoza timu kushinda mechi nne mfululizo na sare moja, jambo lililosababisha wengi kupaza sauti wakitaka apewe nafasi hiyo ya kuwa kocha mkuu wa kudumu.

MANCHESTER, ENGLAND: MJADALA kuhusu mustakabali wa Michael Carrick huko Manchester United unaendelea. Kiungo huyo wa zamani wa Mashetani Wekundu aliteuliwa mwezi uliopita kuchukua nafasi ya Ruben Amorim kama kocha wa mpito hadi mwisho wa msimu.

Lengo lilikuwa Carrick aisaidie klabu kurejesha utulivu kabla ya kuondoka na kumpisha kocha mwenye jina kubwa zaidi. Hata hivyo, Carrick amezidi matarajio hayo kwa kuiongoza timu kushinda mechi nne mfululizo na sare moja, jambo lililosababisha wengi kupaza sauti wakitaka apewe nafasi hiyo ya kuwa kocha mkuu wa kudumu.

Idadi kadhaa ya mastaa wa zamani wa Man United wametoa maoni yao kuhusu uwezekano wa uteuzi huo, baadhi wakisema anastahili moja kwa moja, huku wengine wakisisitiza viongozi wa klabu waendelee na mpango wa awali. Hebu tuangazie  kila mmoja wao alisema nini kuhusu mustakabali wa Carrick na kiti hicho cha moto Old Trafford.


1. Michael Carrick; Tuanzie kwa Carrick mwenyewe. Mara kwa mara ameulizwa kuhusu mtazamo wake juu ya nafasi ya ukocha wa kudumu Man United. Ingawa hilo linaweza kuwa malengo yake, lakini amekuwa makini katika majibu yake. Alisema wiki iliyopita: “Ninafahamu kikamilifu jukumu nililonalo hapa na wajibu wangu. Tunataka mafanikio na nataka klabu iwe na mafanikio hata baada ya mwisho wa msimu, iwe ni mimi au mtu mwingine. Kwa sasa siwezi kudhibiti hilo, tutaona kitakachotokea, lakini muhimu ni kuendelea kuboresha timu na kuifanya Man United iwe imara zaidi. Matokeo ya muda mfupi hayabadili hilo.”


2. Gary Neville; Mchambuzi Gary Neville hajawahi kuogopa kutoa maoni yake kuhusu kinachoendelea Old Trafford na suala la Carrick si tofauti. Baada ya Carrick kupewa kazi hiyo, alisema anapaswa kutimiza jukumu lake la muda tu. Aliposema: “Natumai atafanya vizuri sana. Haipaswi kuwepo mjadala wa kumpa kazi hiyo zaidi ya msimu huu, kwa ajili yake na kwa ajili ya klabu. Hata akishinda kila mechi, tunaweza tukajikuta mwishoni mwa msimu akiwa amefanya vizuri ajabu, mashabiki wakiwa na furaha na timu ikiwa katika nafasi za Ligi ya Mabingwa. Inawezekana. Lakini naamini mwishoni mwa msimu unapaswa kuangalia chaguo kama Pochettino, Tuchel au Ancelotti.”


3. Roy Keane; Roy Keane anaungana na Neville katika kupinga Carrick kupewa nafasi ya kudumu. Awali, alisema Man United inahitaji “kocha zaidi ya bora”. Kisha aliongeza: “Sidhani kama ni uamuzi sahihi, lakini namtakia kila la heri. Kama atapewa kazi hiyo majira ya joto, basi utasema sawa, kila la heri. Lakini kuwa kocha wa mpito ni tofauti na kuwa meneja wa Man United anayepaswa kushinda mataji kwa miaka ijayo. Naamini unaweza kupata kocha bora kuliko Carrick. Anafanya kazi nzuri, mpito umemfaa, lakini kufanya vizuri Man United haimaanishi utafanikiwa kila mahali.”

4. Rio Ferdinand; Ferdinand hakukubaliana na Keane, aliposema: “Haijalishi Carrick atafanya vizuri kiasi gani, bado kutakuwa na hatari kama atapewa kazi hiyo, lakini hilo lipo kwa kila jina linalotajwa. Sielewi kwa nini mtu akipewa nafasi na akafanya vizuri, bado watu waseme hapaswi kupewa kazi hiyo. Sifahamu kwa nini Roy yuko kinyume sana.”


5 .Jaap Stam; Stam alipendekeza Roberto De Zerbi badala ya Carrick, aliposema: “Nampenda sana De Zerbi kwa jinsi alivyofanya Brighton na sasa Marseille. Anacheza soka la kumiliki mpira, anashambulia, anafunga mabao mengi. Ni mzuri pia katika uhusiano na wachezaji. Ningefurahi kama hawatamchagua Carrick na badala yake wamchague De Zerbi.”


6. Dimitar Berbatov; Berbatov anaunga mkono Carrick, lakini anasisitiza subira akisema: “Nina upendeleo kidogo kwa sababu tulicheza pamoja, nataka apate kazi, lakini tusubiri hadi mwisho wa msimu. Tumeona yaliyotokea kwa Ole Gunnar Solskjaer, hivyo tusikimbilie uamuzi. Mwisho wa msimu tutaona.”

Louis Saha; Saha angependa Carrick apewe nafasi ya kudumu wakati aliposema: “Ningependa kuona Michael akipewa nafasi. Amefanya vizuri sana. Anaelewa utamaduni wa klabu, si mgeni. Lakini, majina kama Ancelotti au Zidane yakitajwa, hilo ni suala tofauti kabisa.”


7. Owen Hargreaves; Hargreaves anaamini Carrick anastahili, aliposema: “Sioni kwa nini usimpe kazi hiyo.”

 “Anafanya kazi ya kuvutia. Mashabiki wana furaha, wachezaji wana furaha, na muhimu zaidi timu inashinda. Man United imekuwa na makocha wakubwa kama Van Gaal na Mourinho, lakini jina kubwa halihakikishi mafanikio.”

Carrick ameiongoza Man United kushinda mechi nne mfululizo dhidi ya Manchester City, Arsenal, Fulham na Tottenham Hotspur kabla ya kutoka sare ya bao 1-1 na West Ham United usiku wa Jumanne huko kwenye uwanja wa ugenini jijini London.