Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Shujaa wa Liverpool aingia anga la Rooney

DOGO Pict

Muktasari:

  • Liverpoool ilionekana kama vile imeshamaliza mechi hiyo ya St James' Park wakati ilipofunga mara mbili kupitia kwa Ryan Gravenberch na Hugo Ekitike, huku Newcastle ikimpoteza staa wake Anthony Gordon kwa kadi nyekundu.

LIVERPOOL, ENGLAND: KINDA wa Liverpool, Rio Ngumoha amefuata nyayo za Wayne Rooney kuibeba timu yake wakati akiwa na umri mdogo alipofunga bao dakika ya 100 kusaidia ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Newcastle United uwanjani St James' Park, usiku wa Jumatatu.

Liverpoool ilionekana kama vile imeshamaliza mechi hiyo ya St James' Park wakati ilipofunga mara mbili kupitia kwa Ryan Gravenberch na Hugo Ekitike, huku Newcastle ikimpoteza staa wake Anthony Gordon kwa kadi nyekundu.

Lakini, Newcastle ilipambana licha ya kuwa pungufu uwanjani, lakini ilifunga mara mbili kupitia kwa Bruno Guimaraes na William Osula na kufanya mechi hiyo kuingia kwenye dakika za majeruhi ubao ukisomeka 2-2.

Hata hivyo, wakati Newcastle ikiamini imefanikiwa kunyakua pointi moja kwenye mechi hiyo ya nyumbani dhidi ya mabingwa watetezi, mtokea benchini kinda Ngumoha aliingia na kuwahakikishia Liverpool inaondoka mahali hapo na pointi zote tatu katika dakika 10 za majeruhi.

Hilo ni bao lake la kwanza kwenye kikosi cha wakubwa na sasa Ngumoha akiungana kwenye kundi la kipekee kabisa pamoja na staa wa zamani wa Everton na Manchester United, Wayne Rooney.

Ngumoha anakuwa mchezaji wa pili mwenye umri wa miaka 16 kufunga bao la ushindi katika mchezo wa Ligi Kuu England baada ya Rooney kufanya hivyo kwenye mechi dhidi ya Arsenal wakati huo akiwa Everton mwaka 2002.

Rooney naye alitokea benchini kipindi hicho na kufunga kwa shuti kali lililomshinda kipa David Seaman kuisaidia Everton kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya kikosi cha kocha Arsene Wenger uwanjani Goodison Park.

Akiwa na umri wa miaka 16 na siku 361, Ngumoha ni mkubwa kwa siku moja tu kuzidi Rooney kwa kipindi ambacho alifunga bao hilo dhidi ya Arsenal.

Ngumoha sasa ni mchezaji wanne kinda kufunga bao kwenye Ligi Kuu England baada ya Rooney, James Milner na James Vaughan.

Wakati huo huo, Liverpool imefunga bao katika kila mechi kati ya 36 zilizopita ilizocheza kwenye Ligi Kuu England tangu ilipotoka kapa kwenye kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Nottingham Forest, Septemba 2024.

Liverpool sasa inajiandaa na mechi ngumu kabisa ya kuwakabili mahasimu wao kwenye mbio za ubingwa Arsenal katika kipute cha Anfield, Jumapili.