Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Shughuli EPL kuendelea tena wikiendi hii

EPL Pict

Muktasari:

  • Mechi nyingine, Chelsea itakuwa Stamford Bridge kucheza na Wolves, wakati West Ham itakipiga na Burnley na Everton itamaliza ubishi na Fulham.

LONDON, ENGLAND: ZUBAA ile kwako. Ndicho unachoweza kusema kwenye mchakamchaka wa mikikimikiki ya Ligi Kuu England wikiendi hii, ambapo macho ya wengi yatakuwa huko kwenye kipute cha Tottenham Hotspur na Manchester United na kile cha Manchester City dhidi ya Liverpool. Moto utawaka.

Mapema kabisa Jumamosi, Spurs itajimwaga kwenye uwanja wake wa nyumbani kukipiga na Man United katika moja ya mechi zinazosubiriwa kwa hamu kabisa kutokana na upinzani wa timu hizo kwa miaka ya hivi karibuni. Rekodi za msimu huu, Spurs na Man United zinalingana karibu kila kitu, lakini namba zinaonyesha kwamba katika mechi tano zilizopita kwenye ligi, Spurs imejipigia Man United mara tatu, huku mechi mbili zilizobaki zilimalizika kwa sare.

Kwa maana hiyo, Man United itaingia uwanjani kwenye mechi hiyo ikijaribu kumaliza uteja. Hata hivyo, rekodi za jumla, Spurs na Man United zimekutana mara 66 kwenye Ligi Kuu England, sare zikiwa 14, huku Man United imeshinda 39, mara 15 ugenini na Spurs imeshinda 13, mara nane tu nyumbani. Safari hii itakuwaje? Ngoja tuone.

Kasheshe jingine kubwa zaidi litakuwa Jumapili huko uwanjani Etihad, wakati Man City itakapokipiga na Liverpool katika moja ya mechi za wanaowania ubingwa. Hiyo itakuwa mechi ya 56 kwa miamba hiyo kukutana kwenye ligi, mara 21 zilimalizika kwa sare, huku Man City ikishinda 12, mara 10 nyumbani na Liverpool ikishinda 23, mara tano ugenini. Na rekodi za hivi karibuni, katika mechi tano za mwisho, Liverpool imeshinda mbili, sare mbili na Man City imeshinda moja. Hiki ni kipute cha ubabe mwingi.

Wakati miamba hiyo ikitoana jasho, Arsenal itakuwa na kazi moja tu ya kuendelea kuweka pengo la pointi kwenye kilele cha msimamo wa ligi, wakati itakapokuwa ugenini kucheza na Sunderland. Arsenal imekuwa kwenye kiwango bora sana kwa sasa, ikiwa haijaruhusu bao lolote kwenye nyavu zake kwa mechi nane mfululizo katika michuano yote. Je, itawagomea wapinzani wasiguse wavu wao kwenye mechi hiyo ya Jumamosi? Ni suala la kungoja na kuona.

Namba zinaonyesha Arsenal na Sunderland zimekutana mara 32 kwenye ligi, mara 10 ni sare, huku wenyeji wa mchezo wa leo, wakishinda tatu tu, ambazo ilicheza nyumbani, huku Arsenal ikishinda 19 na mara nane ni katika mechi za ugenini.

Mechi nyingine, Chelsea itakuwa Stamford Bridge kucheza na Wolves, wakati West Ham itakipiga na Burnley na Everton itamaliza ubishi na Fulham.

Mechi za Jumapili, ukiweka kando ile ya kukata na shoka huko Etihad, Aston Villa itacheza na Bournemouth katika moja ya mechi za kibabe sana, huku Brentford ikiwa na kazi mbele ya Newcastle United, Crystal Palace ikicheza na Brighton na Nottingham Forest itaulizana maswali na Leeds United. Ni vuta nikuvute kwenye mchakamchaka huo wa Ligi Kuu England.