Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Safu ya ulinzi Liverpool yamchefua Alejandro Moreno

LIVERPOOL Pict

Muktasari:

  • Udhaifu wa safu ya ulinzi ya Liverpool ulijitokeza tena kwenye mechi hiyo ya Ligi ya EPL, ilipojikuta ikifungwa bao ndani ya dakika tano za mwanzo. 

Mchambuzi Alejandro Moreno, ametoa tathmini kali kuhusu mchezo wa Liverpool kufuatia kichapo cha mabao 3-2 dhidi ya Brentford, akimlenga Milos Kerkez kwa kukosa ushirikiano na beki mwenzake Virgil van Dijk.

Udhaifu wa safu ya ulinzi ya Liverpool ulijitokeza tena kwenye mechi hiyo ya Ligi ya EPL, ilipojikuta ikifungwa bao ndani ya dakika tano za mwanzo. 

Beki wa kati Ibrahima Konaté alihusishwa na kosa lililosababisha bao la pili baada ya kushindwa kumkimbiza Kevin Schade katika shambulizi la kushtukiza. Nahodha Van Dijk naye alisababisha matatizo katika kipindi cha pili kwa kutoa penalti.

Akiwa kwenye majukumu yake ya uchambuzi katika kipindi cha ESPN, Moreno amesema ukosefu wa nguvu ya pamoja ndani ya timu ya Liverpool ulikuwa sababu ya matokeo hayo ya kuumiza kwa mashabiki wa The Reds ambao waliamini timu yao ingeibuka na ushindi jana Jumamosi, Oktoba 25, 2025.

LIVER 01

“Hakuna chachu ya ufanisi katika timu hii kwa sasa,” amesema Moreno. 

“Unaona tabia ya wachezaji wa Brentford wanapozuia shuti la Mo Salah au wanapotuliza hatari wote wanawajibika kwa ushirikiano, walijipongeza kwa kupigiana makofi, walihamasishana kila wakati kufanya kazi ya kuisaidia timu yao. 

“Walifurahia kuwa pamoja. Van Dijk hakuonekana kufurahia hata kidogo kucheza na Kerkez. Kila mara Kerkez alipopiga pasi ya nyuma, Van Dijk alionekana kukerwa na tabia hiyo. Binafsi niliona kama anasema, ‘Ah, uko sawa? Unanitania kweli?’ Hapo ndipo unaona tofauti kati ya timu hizi mbili.”

LIVER 02

Matokeo hayo yalifanya Liverpool kupoteza mechi nne mfululizo za Ligi Kuu kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2021. Pia timu hiyo ya Anfield imeshuka kutoka nafasi ya nne na sasa inashika nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi ya EPL.

Alejandro Moreno raia wa Venezuela, alicheza soka la ushindani katika Ligi kuu ya Marekani (MLS) akiwa na klabu kadhaa.

Alicheza Los Angeles Galaxy  (2002–2004), San Jose Earthquakes (2005),  Houston Dynamo (2006–2007), Columbus Crew (2007–2009), Philadelphia Union (2010) na Chivas USA (2011–2012).

Upande wa timu ya taifa ya Venezuela, Moreno alicheza mechi 41 na kufunga mabao matatu  kuanzia mwaka 2004–2012.