Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Show ya mapumziko yazua mjadala Kombe la Dunia

SHOO Pict

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa wadau wa utangazaji, mapumziko ya mechi hiyo yanaweza kufikia dakika 30, wakati Sheria za Soka zinazoruhusu mapumziko ya kawaida zinaweka kiwango cha juu cha dakika 15 pekee.

DALLAS, MAREKANI: FAINALI ya Kombe la Dunia ya FIFA inatarajiwa kuandika historia kwa kuwa na burudani ya kwanza kabisa ya mapumziko ‘half-time show’, lakini mpango huo umeibua mjadala mkubwa kutokana na uwezekano wa kuvunja sheria za mchezo.

Kwa mujibu wa wadau wa utangazaji, mapumziko ya mechi hiyo yanaweza kufikia dakika 30, wakati Sheria za Soka zinazoruhusu mapumziko ya kawaida zinaweka kiwango cha juu cha dakika 15 pekee.

Burudani hiyo ya aina ya Super Bowl itawakutanisha mastaa wakubwa wa muziki duniani akiwemo Madonna, Shakira, Justin Bieber, BTS, Burna Boy, Gustavo Dudamel pamoja na PS22 Chorus wakishirikiana na bendi ya Coldplay. Ratiba hiyo imeandaliwa na mwimbaji mkuu wa Coldplay, Chris Martin.

Mbali na burudani ya mapumziko, FIFA pia imepanga sherehe kubwa ya ufunguzi itakayoanza dakika 90 kabla ya mechi, ikiwa na mastaa Robbie Williams, Tom Cruise na Nicole Scherzinger.

Iwapo mechi itafika dakika za nyongeza, pamoja na kuwepo kwa mapumziko mawili ya kunywa maji ya dakika tano kila moja, fainali hiyo inaweza kudumu hadi dakika 160 kabla hata ya kuhesabu muda wa majeruhi na mikwaju ya penalti.

FIFA imekataa kutoa maelezo ya ziada kuhusu suala hilo na kusisitiza tu kuwa inalenga burudani ya mapumziko isizidi dakika 11.

Hata hivyo, vyanzo vya ndani vinaeleza kuwa muda huo unaweza kuongezeka kutokana na uchambuzi wa watangazaji pamoja na muda wa kujenga na kuondoa jukwaa la burudani.

Katika Fainali ya Kombe la Dunia la Klabu mwaka jana, mapumziko yalidumu kwa dakika 25.

Mwaka 2021, Bodi ya Kimataifa ya Sheria za Soka (IFAB) ilikataa pendekezo la kuongeza muda wa mapumziko, ikieleza kuwa kufanya hivyo kunaweza kuathiri ustawi na usalama wa wachezaji kutokana na kukaa nje ya mchezo kwa muda mrefu.